Big Sam ameponzwa na haya England

Unknown | 9:17 AM | 0 comments

Chama cha soka nchini England na bosi wa timu ya taifa aliyedumu kibaruani kwa siku 67 tu Sam Allardyce "Big Sam" hatimaye wamekubaliana kuvunja mkataba wa wa Sam kukinoa kikosi hicho cha England.
Sababu zinazotajwa ni mambo ya chini ya kapeti ya Big Sam ambayo yanaweka shaka kwenye uadilifu na uaminifu wake kwa chama cha soka cha Uingereza FA.
www.wapendasoka.com imeongea na mchambuzi wake wa soka la kimataifa, Franck Kimambo ambaye alikua na haya ya kusema.
>>>Big Sam alirekodiwa akiongea na group flani kutoka Far east (mashariki ya mbali) na
kwenye maongezi hayo alinukuliwa akiwasema vibaya Roy Hodgson na Garry Neville kwa jinsi walivyofanya vibaya kwenye Euro na jinsi walivyoaibishwa na Iceland.
>>>Na pia alisikika akisema kua ilikua Ni ujinga kwa FA kutumia pesa nyingi kuukarabati uwanja wa Wembley.
lakini kikubwa kabisa kilichomtimua kazini ni suala la third party.
>>>Third party system ni ile mifumo ya mchezaji kutomilikiwi na timu kwa 100%. Kunakuwa na kampuni pia zinammiliki mchezaji. Kwa hiyo club inakua haina maamuzi ya 100% juu ya mchezaji husika.
>>>Sasa Big sam alirekodiwa kwenye 'hako kakikao' kwa siri akiongea na kampuni fulani kuhusu kuwasaidia kufanikisha hiyo dili na walikubaliana iwapo atawasaidia atalipwa paundi 400,000.
>>>Hii sheria ya third party kwa England ilifungiwa mwaka 2008. Lakini inaonekana kuna njia za panya zinaendelea chini chini na dili zinaendelea na big Sam anazijua.
>>>Katika maongezi Big Sam alisikika akisema kua anaweza kuwaelekeza jinsi ya kufanya na kwamba alipokua kocha wa West Ham alifanikiwa kufanya dili kama hiyo kwa Enne Valencia.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments