TANZANIA YACHAPWA BAO 7 NA IVORY COAST

Unknown | 6:15 AM | 0 comments

Tanzania imeendelea kufanya vibaya katika soka la ufukweni baada ya leo kukubali kichapo cha bao 7-3 toka kwa Ivory Coast.


Mchezo huo wa kuwania kufuzu katika fainali za kombe la mataifa ya Afrika kwa soka la ufukweni ulipigwa katika dimba la Karume ambalo lilitengenezwa kuweza kuendana na dhana kamili ya soka la Ufukweni.

Mpaka mapumziko tayari Tanzania ilishakubali kichapo cha bao 2-1 na kipindi cha pili na cha mwisho hali ilikua mbaya iliyopelekea kufungwa magoli yote hayo.

Mchezo wa marudiano utapigwa Ivory wiki mbili zijazo.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments