ENGLAND WATAJA KIKOSI CHA AWALI CHA EURO 2016

Unknown | 9:53 PM | 0 comments

Kutoka kushoto ni Josh Onomah, Toni Duggan, Harry Kane, Raheem Sterling, Steph Houghton, Nahodha na mfungaji bora wa muda wote, Wayne Rooney na Jordon Ibe wakiwa wamepozi kwa tangazo la jezi za Nike za nyumbani na ugenini za timu ya taifa ya England baada ya kuzinduliwa PICHA ZAIDI GONGA HAPA

KIKOSI CHA ENGLAND 

Makipa: Butland, Forster, Hart
Mabeki: Bertrand, Cahill, Clyne, Jagielka, Rose, Smalling, Stones, Walker
Viungo: Alli, Barkley, Dier, Drinkwater, Henderson, Lallana, Milner, Sterling 
Washambuliaji: Kane, Sturridge, Vardy, Walcott, Welbeck 
Kikosi hiki kitacheza na Ujerumani Machi 26 na Uholanzi Machi 29  
KOCHA Roy Hodgson amemuita kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England kiungo wa Leicester City, Danny Drinkwater wakati akisaka kikosi cha Euro 2016. 
Drinkwater amekuwa na mchango mkubwa kwa mafanikio ya vinara wa Ligi Kuu ya England, Leicester na matunda yake ni kuitwa kwenye kikosi cha maandalizi ya Euro kitakachomenyana mna Ujerumani na Uholanzi katika michezo ya kirafiki mwezi huu.
Kocha Hodgson atatumia mechi hizo mbili kuteua kikosi chake cha mwisho cha wachezaji 23 atakaokwenda nao nchini Ufaransa kwenye Euro 2016, ndani yake akiwarejesha washambuliaji Danny Welbeck na Daniel Sturridge.
"Kazi anayoifanya imeshuhudiwa na kila mtu," amesema Hodgson akimsifia Drinkwater.

Danny Drinkwater ameitwa kwenye kikosi cha England kujiandaa na Euro 2016

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments