VAN GAAL AMTEMA ROONEY, AWABEBA HAWA SAFARI YA DENMARK MECHI YA EUROPA LEAGUE
Morgan Schneiderlin (kulia) na Anthony Martial pichani wakiwa Uwanja wa Ndege wakati wa safari yao leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA
NAHODHA
wa Manchester United, Wayne Rooney ameondolewa kwenye kikosi cha
wachezaji 18 kinachokwenda kumenyana na FC Midtjylland ya Denmark katika
michuano ya Europa League keshi.
Kiungo
Marouane Fellaini amekuwa mchezaji mwingine mzoefu aliyeachwa kwenye
safari hiyo pamoja na beki wa pembeni Matteo Darmian.
Kocha
Louis van Gaal amebeba wachezaji chipukizi zaidi katika safari hiyo,
wakiwemo Regan Poole, Joe Riley na James Weir ambaye anaweza kuchezea
kikosi cha kwanza kwa mara ya kwanza. Credit: Bin zubery
Category: uingereza
0 comments