CHELSEA YAPIGWA VIWILI NA PSG LIGI YA MABINGWA

Unknown | 7:58 AM | 0 comments

Mshambuliaji Edinson Cavani (kulia) akishangilia na David Luiz baada ya kuifungia PSG bao la pili dakika ya 78 katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Chelsea usiku huu Uwanja wa Parc des Princes mjini Paris, Ufaransa. Bao lingine la Paris Saint Germain limefungwa na Zlatan Ibrahimovic dakika ya 39 baada ya shuti lake la mpira wa adhabu kumbabatiza kiungo Mnigeria, John Obi Mikel na kutinga nyavuni. Mikel alifuta makosa yake kwa kuifungia The Blues bao la kusawazisha dakika ya 45 na timu hizo zitarudiana Machi 9, Uwanja wa Stamford Bridge na mshindi wa jumla atakwenda Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya 
PICHA ZAIDI GONGA HAPA

Mshambuliaji wa Benfica, Konstantinos Mitroglou (katikati) akifumua shuti kuifungia bao pekee timu yake ikishinda 1-0 dhidi ya Zenit St Petersburg katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya

No comments:

POST A COMMENT

Note: Only a member of this blog may post a comment.
Pages 22123456 »

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments