MAN CITY MABINGWA WAPYA CAPITAL ONE

Unknown | 7:38 AM | 0 comments

Manchester City imetwaa ubingwa wa ‪kombe la ligi nchini England maarufu kama Capital One Cup‬ 2016 kwa kuifunga Liverpool kwa penati 3-1 katika mchezo wa Fainali uliopigwa katika dimba la Wembley nchini humo.

Katika mchezo huo dakika 120 zilimalizika kwa sare ya bao 1-1 ambapo bao la Man City lilifungwa na Fernandinho dakika ya 49 huku Phillipe Coutinho akiisawazishia Liverpool bao dakika ya 83.
Dakika 30 za ziada zilimalizika bila timu yoyote kuona lango la mwenzake hali iliyolazimu kuingia katika hatua ya mikwaju ya penati.

Emre Can wa Liverpool alianza kufunga penati ya kwanza na baadaye Fernandinho wa Man City kukosa baada ya mkwaju wake kugonga mwamba wa chini.

Baada ya hapo kipa wa Man City Caballero aliibuka shujaa baada ya kuokoa penati 3 mfululizo za Liverpool zilizopigwa na Philipe Coutinho, Lucas Leiva na Adam Lalana huku wapigaji wa Manchester City wakifunga penati zote 3 zilizofuata baada ya kukosa ile ya kwanza.

Yaya Toure ndiye aliyepiga penati ya 4 na kuipa ubingwa huo Man City ambao ni kama zawadi kutoka kwa kocha wao Manuel Pellegrini ambaye anaondoka kikosini hapo baada ya msimu huu kumalizika na kuzima ndoto ya Jurgen Klop ambaye alitaka kuipa Liverpool kikombe cha kwanza tangu ajiunge nao.



Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments