GOLI LA DOGO WA CHELSEA LAMUWEKA KWENYE REKODI YA WAKONGWE
Kinda wa Chelsea ameingia kwenye vichwa vya habari Ulaya baada ya
kutupia kambani bonge la goli kwenye mechi ya U21 kati ya Chelsea dhidi
ya Tottenham.
Ola Aina alifunga goli akiwa kwenye nusu ya uwanja kwa kuachia shuti
kali ambalo lilimshinda golikipa wa Spurs na kutinga wavuni moja kwa
moja.
Kabla ya goli hilo, Chelea ilikuwa mbele kwa magoli 2-0 na goli hilo
likaendelea kuiweka mbele Chelsea kwa magoli 3-0 kwenye mchezo huo.
Goli hilo limemfanya Ola Aina ameingia kwenye orodha ya mastar
wengine kama David Beckham na Xabi Alonso ambao wamewahi kufunga magoli
kama hayo siku za nyuma.
Unaweza kujiuliza maswali mengi kwamba ilikuwaje golikipa akafungwa
goli kama hilo, lakini ni vizuri uangalie mwenye namna ambavyo dogo
aiingia kwenye rekodi ya wakongwe wa soka duniani.
Category: uingereza
0 comments