MAN UNITED VITANI NA BAYERN MUNICH KUWANIA SAINI YA SADIO MANE
KLABU
ya Manchester United inakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Bayern
Munich katika kuwania saini ya mshambuliaji, Sadio Mane.
Mpachika
mabao huyo wa Southampton amekuwa lulu Ulaya baada ya kazi nzuri
aliyoifanya katika miezi yake 18 ya kufanya kazi St Mary’s.
Na
vigogo wa Ujerumani, Bayern ni klabu nyingine inayojitokeza sasa
kumuwania mshambulkiaji huyo, ambaye amefunga mabao 17 katika kikosi cha
Ronald Koeman tangu awasili msimu uliopita. Chelsea pia nayo inamtaka
kwa 'udi na uvumba' mkali huyo wa mabao.
Klabu za Manchester United na Bayern Munich zinagombea saini ya winga wa Southampton, Sadio Mane
Mane anataka sana kwenda Old Trafford, lakini inafahamika Southampton haiko tayari kumuuza, labda dau la ada ya uhamisho la Pauni Milioni 40 liwekwe mezani.
Bin Zubery
Category: uingereza
0 comments