MABONDIA THOMASI MASHALI NA FRANSIC CHEKA WATAMBIANA,KUZICHAPA DESEMBA 25 MOROGORO

Unknown | 7:28 PM | 0 comments



Mabondia Thomas Mashali kushoto na Fransic Cheka wakitunishiana misuli wakati wa kutambulisha mpambono wao utakaofanyika katika uwanja wa jamuhuri Morogoro Desemba 25 Picha na SUPER D BOXING NEWS

Mabondia Thomas Mashali kushoto na Fransic Cheka wakitambiana mbele ya wandishi wa habari wakati wa kutambulisha mpambano wao wa desemba 25 utakaofanyika katika uwanja wa jamuhuri Morogoro .
Bondia Thomas Mashali kulia akizungumza na waandishi wa habari awapo pichani wakati alipokuwa akitambulisha mpambano wake na Fransic Cheka kushoto utakaofanyika katika uwanja wa jamuhuri Morogoro siku ya Desemba 25 .

Mabondia Fransic Cheka kushoto na Thomas Mashali wakiangaliana kwa usongo wakati wa kutambulisha mpambano wao wa desemba 25 utakaofanyika katika uwanja wa jamuhuri Morogoro
KOCHA WA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI RAMADHANI UHADI KULIA AKIWA NA PROMOTA KAIKE SIRAJU PAMOJA NA BONDIA THOMAS MASHALI Mabondia Thomas Mashali kushoto na Fransic Cheka wakitambiana mbele ya wandishi wa habari wakati wa kutambulisha mpambano wao wa desemba 25 utakaofanyika katika uwanja wa jamuhuri Morogoro
Na Mwandishi Wetu

MABONDIA Thomas Mashali wa Dar es salaam na Fransic Cheka wa Morogoro wamendelea kutambiana kuelekea mpambano wao wa desemba 25 utakaofanyika katika uwanja wa jamuhuri Morogoro uzito wa kg 76

akiongea na waandishi wa habari Mashali amesema kuwa hii ni vita ya Dar na Moro hivyo kawaomba wapenzi wa mchezo wa masumbwi wa Dar es salaam waweze kuhamia morogoro kwa muda kwa ajili ya kumsapoti

siku hiyo ambayo kwake atakuwa na kibaruwa kigumu ambapo atapigana na Cheka pamoja na wakazi wa Morogoro nae Chaka alijibu mapigo hayo kwa kusema siku zote anamweshimu bondia anaetaka mpambano wa marudiano hata hivyo dozi ya mashali ipo pale pale na nitampiga katika raundi za awali tu kwa kuwa nipo vizuri na naendelea na mazoezi

nae kocha wa Mashali Ramadhani Uhadi amesema kuwa cheka ni bondia wa kawaida sana hivyo wapenzi waje waone mchezo mzuri utakaochezwa na Mashali atakavyo msambalatisha Cheka siku hiyo mjini Morogoro na kocha wa bondia Cheka Abdallah Salehe amesema Cheka yupo vizuri sana kwa sasa nimempika ameshaiva ata kama mpambano utakuwa leo Mashali atapigwa mapema sana

katika mpambano huo kutakuwa na mipambano mingine ya bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' atapambana na Twaha Kassimu kg 63 na Vicent Mbilinyi kg 63 atakumbana na Deo Njiku wakati Pius Kazaula kg 66 atamenyana na Seba Temba mpambano mwingine utawakutanisha mabondia Epson John kg 57 na Sadiq Momba na wana dada Lulu Kayage kg 51 atapambana na Mwanne Haji kugombania ubingwa wa taifa

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments