Hawa ni maofisa wengine wa FIFA waliokumbwa na kashfa ya rushwa…

Unknown | 7:48 PM | 0 comments


Alfredo Hawit


Bado hali si shwari ndani ya Shirikisho la soka la mpira wa miguu duniani FIFA, baada ya kusimamishwa kwa aliyekuwa Rais wa shirikisho hilo Sepp Blatter na viongozi wengine, headlines zimerudi tena!!.
Kuna maofisa kutoka Shirikisho hilo wamekamatwa na askari kutokana na msako uliofanywa asubuhi ya leo kwenye moja ya hoteli ya Baur Au Lac, huko Zurich, Uswis, wakihofiwa kupanga njama za kupokea rushwa ndani ya Hotel hiyo.
FIFA imethibitisha kuwa, Makamu wa rais, Alfredo Hawit kutoka Honduras na Juan Angel Napout wa Paraguay ni moja ya maafisa waliokamatwa na hii ni mara ya pili sasa kwa maafisa hao kutumia Hotel hiyo kama sehemu ya makutano.
Alfredo Hawit
Alfredo Hawit (aliyekaa katikati) ni mmoja kati ya Makamu wa rais wa FIFA, aliyekamatwa kwenye hotel hiyo.
FIFA wamesema wataendelea kufuatilia kwa kushirikiana na Marekani, kufanya uchunguzi wa kina ambao unaendeshwa na Ofisi ya mwanasheria mkuu wa Uswis, kama ambavyo inakubalika na sheria ya Uswis na kwa sasa haitazungumza lolote juu ya tukio hilo mpaka uchunguzi utakapokamilika.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments