RAIS VLADMIR PUTIN WA URUSI AFUNGUA RASMI MICHEZO YA SOCHI

Unknown | 8:54 PM | 0 comments

 

Sochi 2014 Opening CeremonyRais Vladmir Putin wa Urusi amefungua rasmi mashindano ya olimpiki ya msimu wa baridi katika mji wa utalii wa Socchi katika sherehe iliyofana.
Waliokuwa wanariadha mashuhuri nchini Urusi waliubeba mwenge wa Olimpiki kabla ya kuwashwa na aliyekuwa mlinda lango wa mchezo ya magongo Vladislav Tretiak pamoja na Mchoraji wa barafu Irina Rodnina.
Awali mashabiki waliongozwa katika sherehe iliofana kuhusu historia ya Urusi na mchango wake ulimwenguni.
Katika siku 16 zijazo,karibia wanariadha 3000 watashiriki katika michezo 98 tofauti katika mashindano hayo yaliodaiwa kugharimu takriban dola billioni 50.
       

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments