Newcastle wafanikiwa kupata saini ya De Jong
Klabu
ya Newcastle imefanikiwa kumsajili mshambuliaji,Luuk De Jong kutoka
Borussia Monchengladbach kwa mkopo katika kipindi kilichosalia cha msimu
na baadae kumnunua moja kwa moja majira ya joto.
Mabata
weusi hao wapo katika mipango ya kupata saini ya kiungo wa Lyon,Clement
Grenier kwaajili ya kuziba nafasi ya Yohan Cabaye aliyesajiliwa na
Paris St Germain kwa kiasi cha paun milioni 20.Raia
huyo wa Ufaransa ambaye ana umri wa miaka 23,alishawahi kukiri kuwa
anataka kuondoka Lyon na kujiunga na Arsenal iliyoonyesha nia ya
kumtaka.De Jong mwenye umri wa miaka 23 raia wa Uholanzi aliyekuwa akiichezea FC Twente kabla ya kuhamia Ujerumani mwaka 2012 atakuwa akivaa jezi namba 18 na anataraji kucheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Sunderland Jumamosi.
Category: uingereza
0 comments