Matokeo ya Simba na Rhino Rangers haya hapa.
Mechi
kati Simba na Rhino Rangers imemalizika kwa ushindi wa goli 1 la Simba
dhidi ya 0 kwa Rhino Rangers kwenye mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara mechi iliyomalizika jioni hii Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam.
Kwa Ushindi huu unaifanya timu ya Simba SC itimize pointi 28 baada ya
kucheza mechi 14 ikibaki nafasi ya 4 nyuma ya Yanga ambayo yenye pointi
31 Azam na Mbeya City pointi 30 kila moja.
Hadi mapumziko tayari Simba SC walikuwa wanaongoza kwa goli 1-0
lililofungwa na mshambuliaji Ramadhani Yahya Singano ‘Messi’ dakika ya
14
Pamoja na kufungwa Rhino walionekana kucheza vizuri na kuonyesha
upinzani kwa Simba ambao katika mechi ya mzunguko wa kwanza walitoka
nayo sare ya 2-2 mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Ally Hassan Mwinyhi
Tabora.
Kikosi cha Simba SC leo kilikuwa na wachezaji wafuatao; Ivo Mapunda,
Haruna Shamte, Idrisa Rashid, Gilbert Kaze, Donald Mosoti, Awadh Juma,
Haruna Chanongo, Amri Kiemba, Ali Badru/Said Ndemla dk, Amisi
Tambwe/Betram Mombeki aliyeingia dk65/Henry Joseph aliyeingia dk85 na
Ramadhani Singano ‘Messi’.
Kwa upande wa Rhino Rangers wachezaji wake walikua ni; Charles
Mpinuki, Julius Masunga, Amani Juma, Ladislaus Mbogo, Laban Kambole,
Hamisi Msafiri, Salum Kamana, Hussein Abdallah, Darlingtn Enyinna,
Suleiman Jingo/Salum Majid dk84 na Shijja Mongo.
Category: tanzania
0 comments