Chelsea vs Man City – Arsenal vs Liverpool kombe la FA raundi ya tano
Chelsea wamepangiwa kucheza na Manchester City katika mchezo
unaotazimiwa na ushindani wa hali ya juu katika mfululizo wa michuano ya
kombe la FA Cup.
Chelsea ambao wamefuzu kwenye raundi ya tano kwa kuiondosha Stoke
City katika mchezo ambao ulimalizika kwa ushindi wa bao moja kwa bila.
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho akizungumza punde baada ya droo hii
amesema, “Iwapo unataka kuwa bora lazima ucheze na timu bora.”
Nao Manchester City wao walijikatia tiketi ya kufuzu michuano hiyo hatua ya tano kwa kuiadhibu Watford kwa mabao 4-2.
Liverpool wao watakuwa wageni wa Arsenal kwenye mchezo wa raundi ya tano.
Roberto Martinez ataiongoza Everton kukutana na timu yake ya zamani
ya Swansea, ilihali Sunderland wao watacheza na Southampton ikiwa ni
mechi liyokutanisha timu zote za ligi ya England.
Cardiff watakuwa nyumbani kuwakaribisha Wigan na Hull watacheza na
Brighton. Sheffield Wednesday watapamabana na wenzao walioko kwenye ligi
ya Championship, Charlton FC.
Mechi zote zitachezwa jumamosi na jumapili ya tarehe 15 na 16 mwezi wa pili.
Mshindi wa mechi kati ya Fulham ama Sheffield United atapambana na
mshindi kati ya Nottingham Forest au Preston kwenye hatua ya raundi ya
tano ya kombe hilo ambalo fainal yake itachezwa kwenye uwanja wa
Wembley.
Category: uingereza
0 comments