YAYA TOURE MCHEZAJI BORA AFRIKA WA TUZO YA BBC

Unknown | 11:52 PM | 0 comments




Yaya Toure amechaguliwa kuwa mchezaji bora Afrika wa tuzo ya BBC 2013.
Msimu uliopita, yaani mwaka jana mwezi kama huu, Mzambia Christopher Katongo alitangazwa kushinda tuzo hiyo.

Kiungo huyo wa Manchester City na Ivory Coast ametwaa tuzo hiyo kwa kuwapiku Pierre-Emerick Aubameyang, Victor Moses, John Mikel Obi na Jonathan Pitroipa .
KUTOKA KUSHOTO; AUBAMEYANG, PITROIPA, OBI, MOSES NA YAYA.

Yaya mwenye miaka 30, ameiambia BBC kuwa: “Nimeteuliwa kwa miaka minne bila ya kushinda, safari hii ni mara ya tano na nimeshinda, ni kitu cha aina yake.”
 “Nina furaha kubwa kufanikiwa kushinda tuzo hii kubwa na ninatoa shukurani zangu kwa waandaaji.

"Najua kuna wachezaji wengi bora barani Afrika mfano kama Aubameyang, Pitroipa, Mikel, Moses, Salomon Kalou, Gervinho na wengine wengi lakini leo nimeshinda.”

Yaya pia alilisifia bara la Afrika kwa kuendelea kuzalisha vipaji na mpira wake kuendelea kupiga hatua.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments