WANACHAMA ZAIDI YA 400 WA SIMBA WATUA BUNGENI KUSHINIKIZA RAGE AJIUZULU SIMBA

Unknown | 9:07 AM | 0 comments


Zaidi ya wanachama 400 kutoka matawi mbalimbali ya klabu ya simba wamefunga safari kutoka jijini Dar es salaa mpaka bungeni mjini Dodoma wakimtaka spika wa bunge Anne Makinda amfikishe kwenye kamati ya maadili ya bunge mwenyekiti wa klabu hiyo Ismail Aden Rage ambaye pia ni mbunge jimbo la tabora mjini kwa madai ya kukiuka katiba ya simba na kuendesha klabu hiyo kibabe kinyume na sheria za nchi zinavyoelekeza.

ITV ilifika nje ya viwanja vya bunge na kushuhudia baadhi ya wanachama waliowawakilisha wenzao wakipiga kambi nje ya bunge kumsubiri spika wa bunge ili kufikisha kilio chao ambapo wamesema wamechoshwa na kile wanachodai mwenyekiti wa Simba Ismail Rage kuisigina katiba ya klabu hiyo kwa maslahi yake binafsi ilhali akijua klabu hiyo imesajiliwa kwa mujibu wa sheria za nchi ambazo hutungwa na chombo hicho cha kutunga sheria cha bunge.

Hata hivyo wanachama hao hawakufanikiwa kufikisha ujumbe wao kutokana na kutozingatia taratibu za bunge na kuahidi kurejea jijini Dar es Salaam kujipanga upya ambapo jitihada za ITV kumtafuta mwenyekiti Rage ili kuzungumzia hatua ya wanachama hao ziligonga mwamba kutokana na mbunge huyo kudaiwa kuwa safarini kikazi.

ITV

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments