WAHUSIKA WAWAJIBIKE KUTEGUA KITENDALIWI CHA OKWI KWA MASHABIKI WA SIMBA…MWANASHERIA NDUMBARO AFUMUA UKWELI!!

Unknown | 10:04 PM | 0 comments

 

Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe, Dar es salaam
Tel: 0712461976 au 0764302956
SIKU kadhaa baada ya Yanga kutangaza kumsajili mchezaji hatari kutoka SC Villa ya Uganda, Emmanuel Anord Okwi, wanachama wa klabu ya Simba sc na wadau wa michezo wameshindwa kutegua kitendawili cha nani  mmiliki wa  mchezaji huyo kati ya Etoile Du Sahel ya Tunisia na SC Villa ya Uganda.
Wakati wote wamekuwa wakipiga simu na kutuma ujumbe mfupi wa simu wakihitaji ufafanuzi juu ya sakata hili ambalo ndio habari ya mjini kwa sasa. Kila kona ni usajili wa Okwi kwenda Yanga.
Yanga wakati wanatangaza kumsajili okwi, mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya klabu hiyo, Abdallah Ahmed Bin Kleb alisema wamefuata tararibu zote na kujiridhisha kuwa wapo sahihi kumsajili Okwi.
Bin Kleb alienda mbali zaidi na kusema wamewaona wanasheria, wamefuatilia hadi FIFA na kupata hati ya hukumu ya  Okwi kushinda kesi dhidi ya klabu yake ya Etoile ambayo alikuwa anadai haijamlipa mshahara wake kwa miezi mitatu pamoja na baadhi ya hela za uhamisho wake.
“Tulimsajili Okwi  na mpaka sasa tumepata  Hati yake ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) na ndio maana tumeweka mambo hadharani”. Alisema Bin Kleb siku akitangaza usajili wa Okwi.
Okwi aliuzwa na Simba kwenda klabu ya Etoile Du sahel ya Tunisia januari mwaka huu kwa kitita cha dola 300, 000 za kimarekani, lakini hakudumu katika klabu hiyo kwa madai ya kutolipwa haki zake na kuamua kurejea kwao Uganda.
Okwi baada ya kurejea kwao Uganda alikaa miezi sita bila kucheza na ndipo shirikisho la  kandanda la Uganda (FUFA) likasimama kidete kumpigania aruhusiwe kureja nyumbani na kujiunga na Sport Club Villa ya Uganda `Majogoo wa Kampala`  ili kulinda kiwango chake.
Okwi
Watu wamevurugwa: Okwi amewaacha hoi mashabiki wa Simba sc, hawaelewi nini kinaendelea, Yanga wachekelea usajili wake.
Okwi ni mchezaji wa Etoile inayodaiwa na Simba Sc kitita cha dola za kimarekani 300,000 na sakata hilo limefika mpaka FIFA.
Wakati Yanga wakisema wamejiridhisha kumsajili Okwi na kuona wako sahihi, Simba nao wanazungumza yao wakisema watani wao wa jadi wamejipalia mkaa kwa usajili wa mchezaji huyo.
Mwenyikiti wa kamati ya usajilli ya Simba, Kaptein Zacharia Hans Poppe alisema Okwi ni mchezaji halali wa Etoile na kama Yanga wamemsajili bila mawasiliano na klabu hiii na kudanganywa na Villa ambayo ilikuwa inamtumia mchezaji kwa mkopo wa miezi sita tu, basi wameingia `shimo la tewa.`.
Poppe aliongeza kuwa shirikisho la soka nchini Uganda lilitaka kumtumia mchezaji huyo kwenye fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani, lakini wakagonga mwamba baada ya kuambiwa haiwezekani kwani ni mchezaji halali wa Etoile Du Sahel.
Yanga wanajilinda zaidi na kueleza kuwa wameshafika FIFA na kupewa hati ya hukumu ya kesi ya Okwi na klabu yake , ambapo Okwi kupitia kwa wakili wake aliishitaki timu hiyo kwa kutomlipa fedha zake zikiwemo za mshahara, baadaye alishinda na kuruhusiwa kuvunja mkataba wake.
Kuna wakati iliwahi kuelezwa na Simba sc Kuwa Okwi aliruhusiwa na klabu yake kwenda Uganda kuitumikia timu yake ya Taifa, lakini alichelewa kurejea Tunisia na klabu ikampa adhabu ya kukatwa mishara ya miezi yoye ambayo hakuwepo kazini.
okwi2
Okwi akiwa Simba enzi zake, alikuwa fundi vibaya mno
Pia alishushwa akafanye mazoezi na timu ya pili , lakini kama ilivyo kawaida kwa Mganda huyo akapiga chini mpango na kuaanza kula bata tu mpaka alipoamua kurejea kwao Uganda.
Hapa ndipo mgogoro wa Etoile na Okwi ulipoanzia, lakini alipoenda kwao Uganda alikuwa anakaa tu kwa miezi sita na ndipo FUFA wakaona ni busara kumwombea ruhusa maalumu ya kucheza Villa ili kunusuru kiwango chake.
Amecheza Villa kwa miezi kadhaa mpaka alipotangazwa kusajiliwa na Yanga desemba 15 mwaka huu zikiwa zimesalia saa chache kufunga dirisha dogo la usajili.
Baada ya kutoka kwa habari hii iliyogonga vichwa wa watu wengi, nimepokea simu nyingi sana, kila mtu anataka ufafanuzi juu ya usajili huu anaookena kuwa na utata.
Tatizo linaloonekana si Yanga imempataje mchezaji huyo?, watu wengi wanajiuliza nani ni mmiliki wa Okwi?.
Kama Etoile walimruhusu Okwi akacheze Villa kwa Mkopo halafu wamemuuza imekuwaje”
Je, kuna mazungumzo kati ya Villa na Etoile juu ya mchezaji huyu?. Pia Etoile wameilipa Simba fedha zake za mauzo?.
Yapo maswali mengi yanayoulizwa na wasomaji juu ya usajili huu huku wakitaka kujua Kama ni kweli Simba hawajalipwa fedha za Okwi. kama wamelipwa nani kazipokea?. Kwanini Villa waruhusiwe kumuuza mchezaji ambaye yupo kwa mkopo klabuni kwao  tena kwa ruhusa maalumu ya FIFA?.
Kwa sasa kuna mfumo wa Transfer Matching System (TMS). Kwa kutumia mfumo wa Kisasa jina la mchezaji mwenye matatizo lisingeweza kukubali kuingia katika orodha ya wachezaji wa Dar Young Africans.
Swali la Msingi, imekuwaje Yanga wamefanikiwa kuliingiza jina la Okwi? Kwa nini wamepata ITC kama kweli Okwi alikuwa ana matatizo?. FUFA wametoa ITC wakijua Okwi  ana matatizo?. Maswali ni mengi sana ambayo wadau wa soka wanataka ufafanuzi.
Mtandao huu ulikutana na mwanasheria ambaye ni wakala wa kimataifa wa wachezaji, Dokta Damans Ndumbaro ambaye alifafanua kuwa ITC inatolewa na shirikisho la nchi inayochezea kwa wakati husika.
Kwa tafsiri hiyo, Okwi alikuwa anachezea Uganda na ndio maana FUFA wametoa ITC.
Lakini Ndumbaro aliongeza kuwa FIFA hawatoi ITC, isipokuwa wanakuwa wanaangalia machakato mzima wa ITC ile.
Ndumbaro aliongeza kuwa shirikisho la nchi  husika linaweza kutoa ITC kwa mchezaji hata kama ana matatizo, ila itategemeana na mazingira ya wakati huu.
“Tatizo la Okwi lipo Tunisia, kama SC Villa wameelewana na Etoile basi hakuna tatizo. Lakini kama hawana mawasiliano na wao wamemuuza mchezaji  aliyekuwa kwa mkopo tu bila ridhaa yao, basi huo ni UTAPELI” na lazima wawajibike kwa mujibu wa sheria. Alisisitiza Dkt. Ndumbaro.
Kama nilivyosema awali, tatizo si  Yanga kumsajili Okwi, tatizo lipo katika mfumo uliotumika. Kuna watu wanawajibika kutegua kitendawili hiki.
Kama kweli Okwi alishinda kesi FIFA, hakika Yanga wanatakiwa kutoa vielelezo zaidi vinavyothitibisha uhalali wa wao kumsajili nyota huyo ikiwemo hiyo hati ya hukumu  waliyosema wanayo.
DSCN9881
Anakwenda FIFA: Mwenyekiti wa Simba Sc, Ismail Aden Rage amesema anakwenda FIFA kuhusu suala la Okwi
Sheria za FIFA ziko wazi kuwa klabu inatakiwa kuwa imemaliza kulipa malipo ya fedha za kumnunua mchezaji kabla ya kumaliza Mkataba wake au kumtoa sehemu nyingine, sasa Etoile watalazimika kuilipa Simba SC mara moja kama walishindwa kesi na Okwi. Hakika Deni halifutiki, lazima dola 300,000 zilipwe kwa Simba sc.
Pia tunatarajia TFF Kumaliza suala hili. Tunafahamu wanao mfumo mzuri wa kumuidhinisha mchezaji kuichezea klabu husika, wadau wawe na subira kidogo.
TFF watawasiliana na FIFA na kupewa vielelezo vyota vya Okwi na uhalali wa Yanga kumsajili, baada ya hapo wataamua kumuidhinisha kuitumia Yanga kama wamefuata taratibu au kutoruhusiwa kuichezea klabu hiyo kama kuna Matatizo.
Mbwembwe-za-mashabiki-wa-timu-ya-Simba-Dar-es-Salaam-wakishangilia-katika-pambano-lao-na-Kiyovu-jana-jijini-Dar-es-Salaam.-Picha-na-Blog-ya-Father-Kidevu
Wengi wao wameduwaa tu, eti wahawaelewi suala la Okwi
Kwasasa imekuwa ngumu kupata maelezo kutoka kwa Etoile Du Sahel juu ya sakata lao na Okwi pamoja na Simba sc, lakini siku si nyingi ukweli utafahamika.
Kwa wale wanaoendelea kupiga simu na kunitumia ujumbe mfupi, hususani mashabiki wa Simba sc, kikubwa ni wao kuwa watulivu, kwa mazingira niliyosema hapo juu, dola zao 300,000 kama hazijaliwa zitalipwa tu, lakini kama zilishalipwa hapo ni tatizo lingiine.
Mwenyekiti wao Aden Rage tayari ameshasema uongozi umeandika barua kwenda FIFA kuhusu madai yao ya dola 300,000 kwa klabu ya Etoile Du Sahel.
Kama kuna siasa ndani ya suala hili ni jukumu la wanachama kumhoji mwenyekiti wao ili kuondoa utata wa fedha za mauzo ya Okwi.
Sheria zipo na siku zote huwa zinaweka mambo sawa.. Zipo wazi na zinaeleza nini kifanyike, kwahiyo swala la usajili wa Okwi litatolewa ufumbuzi kwani wahusika  wapo kwa ajili ya kazi ya kutoa ufafanuzi juu ya nini kimefanyika mpaka Yanga kumsajili.
Karibu sana kwa maoni na maswali
Baraka Mpenja
Tel: 0712461976

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments