WADAU WA MCHEZO WA KIKAPU NCHINI TANZANIA WAIOMBA SERIKALI KUUSIMAMISHA UCHAGUZI MKUU WA CHAMA HICHO.

Unknown | 10:14 PM | 0 comments


 Mchezaji nguli na kocha wa mpira wa kikapu,Bahati Mgunda akizungumza na waandishi wa habari hii leo juu ya azima yake ya kuiomba serikali kuingilia kati uchaguzi wa chama cha mchezo wa kikapu nchini (TBF ).
 Naye kocha wa timu ya Taifa ya mchezo huo mzawa Robert Manyerere naye alikuepo kwenye mkutano huo wa waandishi wa habari uliofanyika kwenye mgahawa wa Hadees jijini Dar Es Salaam.
BARUA YA WAZI KWENDA BMT
YAH: OMBI LA KUSIMAMISHA UCHAGUZI MKUU WA SHIRIKISHO LA MPIRA WA KIKAPU TANZANIA (TBF).

Tafadhari rejea kichwa cha habari hapo juu.
Kwa nafasi yangu ya Ualimu/ Coach wa Timu ya Taifa ya Mpira wa Kikapu (Wanume) Tanzania, Nakuandikia barua hii ya wazi Kwa nia njema kabisa yenye maombi 2 kwako likiwemo la kusimamisha zoezi zima uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwezi baada ya kugundua kuwa kuna ukiukaji mkubwa wa katiba ya TBF ambayo inatoa maagizo juu ya usimamiaji na utekelezaji mzima wa zoezi hilo. BMT kama msimamiaji mkuu wa michezo naamini unayonafasi nzuri ya kuzuia matatizo kabla hayajajitokeza kama ambavyo inaelekea katika zoezi zima la uchaguzi wa TBF. Maombi yangu makuu ni haya yafuatayo

1: Kusimamisha zoezi zima la uchaguzi kwani linakiuka na kwenda kinyume na Katiba ya TBF. Ibara ya 17, 18, 19 na 20

2: Kufanyike uhakiki wa wanachama wa TBF kuelekea Mkutano mkuu wa Bodi wenye jukumu la Kuandaa na kutangaza tarehe ya Mkutano mkuu wa uchaguzi..

1: KUSIMAMISHA ZOEZI ZIMA LA UCHAGUZI KWANI LINAKIUKA NA KWENDA KINYUME NA KATIBA YA TBF. IBARA YA 6, 7, 8, 9, 17, 18, 19 NA 20

Nimeambatanisha sehemu ya katiba Ibara ya 17, 18, 19 na 20 . (ukurasa wa 3-6 wa barua hii)
Kwa mazingira yaliyopo sasa inaonekana mkutano mkuu umeitwa au kuandaliwa na kamati ya utendaji badala ya Bodi ya shirikisho. Kamati ya utendaji inabidi iwajibike kwenye Bodi kitu amabacho hakijafanyika na baada ya hapo inabidi uitishwe mkutano mkuu ambao utaridhia maamuzi ya Bodi ikiwa ni pamoja na kukubaliana juu ya mkutano mkuu wa uchaguzi.

Kwa sasa Katibu mkuu ambaye kikatiba ndie mwenyekiti wa Kamati ya utendaji (Ibara ya 18 na 20) amesimamishwa na Kamati hiyo hiyo kitu ambacho ni kinyume na kazi za kamati hiyo.
Mtafaruku mwingine ni wasiwasi juu ya uhalali wa baadhi ya maamuzi ya kamati hiyo ambapo Rais na makamu wake si wajumbe ila wanaweza kualikwa tu na hawana haki ya kupiga kura katika maamuzi ya kamati ya utendaji. Nina wasiwasi mkubwa sana juu ya kutimia kwa wajumbe (nusu ya wajumbe wa kamati ya utendaji ili uwepo uhalali wa vikao vya kamati ya utendaji) kuelekea maamuzi yanayotolewa. Pamoja na mapungufu hayo lakini ili kuondoa mtafaruku basi kamati ya utendaji iwajibike kwanza kupeleka taarifa zake zikajadiliwe kenye Bodi na bodi ndio iridhie kuwepo kwa Mkutano mkuu na mkutano mkuu wa uchaguzi..

2: KUFANYIKE UHAKIKI WA WANACHAMA WA TBF KUELEKEA MKUTANO MKUU WA BODI WENYE JUKUMU LA KUANDAA NA KUTANGAZA TAREHE YA MKUTANO MKUU WA UCHAGUZI..

Hapa ninaomba BMT kwa kushirikiana na Msajiri wa Vyama vya michezo hapa Tanzania kufuatilia uhalali wa vyama vya mpira wa kikapu vya mikoa kama kweli vipo kihalali kwani kimsingi vyama hivyo ni wanchama wa msingi wa TBF. Toafauti na inavyofanyika sasa ambapo vimekuwa vikijitokeza tu wakati wa mkutano mkuu wa uchaguzi na watu kupeana madaraka ili wakapige kura sio kuendeleza mchezo katika mikoa yao. Nimeambatanisha nakala kuonyesha Ibara ya 6, 7, 8 na 9 ya katiba ya TBF inayoelezea wanachama na majukumu yao.

NI matumaini yangu kuwa utalifuatilia swala hili ili kurekebisha taratibu zilizo kiukwa na baadae kuruhusu au kusimamia taratibu za Uchaguzi kwa mujibu wa sheria na Katiba ya TBF. Hii ni kwa faida ya maendeleo ya mchezo huu hapa Tanzania na itapelekea kupata muda mzuri wa wanaogombea uongozi kujitokeza, wajumbe kupata nafasi ya kujadili ajenda, kuwatambua wagombea na kuandaa maswali wakati wa uchaguzi. Kwa mazingira yaliyopo sasa muda uliowekwa kwa ajiri ya mkutano mkuu/Bodi na mkutano mkuu wa uchaguzi haviwezi kufanyika kwa siku moja au mbili zinzofuatana. Naamini kuna mengi ya kujadiliwa kabla ya mkutano mkuu wa uchaguzi. Wanachama wapewe muda wa siku 30 baada ya tangazo la mkutano mkuu ajenda ikiwa ni moja kuelekea mkutano mkuu wa uchaguzi. Kwa kufanya hivyo naamini kutakuwa na muda mzuri wa kufanya kampeni na kuwashawishi wajumbe kama ambavyo imekuwa ikifanyika katika vyama vingine ambavyo BMT mmekuwa mkisimamia chaguzi zao.

Asante.

Wako michezoni,



Kocha BAHATI MOSES MGUNDA.

NAKALA:
1: TANZANIA BASKETBALL FEDERATION
2: MSAJIRI WA VYAMA VYA MICHEZO TANZANIA
3: VYOMBO VYA HABARI

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments