TANZANITE YAKUBALI KICHAPO CHA MABAO 4-1 DHIDI YA WATOTO WA MANDELA

Unknown | 10:41 PM | 0 comments




Mshambuliaji wa Tanzanite, Shelda Boniface (kushoto) akijaribu kumtoka beki wa Afrika ya Kusini, Meagan Newman, wakaati wa mchezo wa kuwania kufuzu kucheza michuano ya Kombe la Dunia kwa wanawake chini ya umri wa miaka 20, uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Saalm, leo jioni. Katika mchezo huo Afrika ya Kusini ilishinda mabao 4-1. 
*********************************************
 TIMU ya wanawake chini ya umri wa miaka 20 ya Tanzania 'Tanzanite' leo imefungwa jumla ya mabao 4-1 na Afrika Kusini 'Basetsana' kwenye mchezo wa raundi ya pili ya  kuwania kufuzu kucheza kombe la dunia mwakani nchini Canada kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Afrika Kusini ilianza vyema mchezo huo kwa  kuwazidi  ujanja Tanzanite katika kipindi cha kwanza cha mchezo baada ya kuzitumia vizuri nafasi walizopata kwa kufunga bao la kwanza dakika ya nne ya kipindi cha kwanza kupitia kwa mchezaji wake Amogelang Motay.

Bao hilo liliamsha mashambulizi  makali kwa Tanzanite waliokuwa wakitafuta nafasi ya kusawazisha ambapo dakika ya 13 walifanikiwa kusawazisha kupitia kwa Theresa Yohana aliyepiga shuti kali la mita kama 30 na kumwacha kipa wa Afrika ya Kusini akiduwaa.
Mashambulizi yaliendelea pande zote mbili, ambapo dakika ya 17 mchezaji wa Afrika Kusini Shiwe Nogwanya, aliipatia timu yake bao la pili lililodumu hadi mapumziko.

Baada ya mapumziko timu zote zilikuwa zikifanya mashambulizi  lakini Afrika Kusini waliendeleza mashambulizi yao upande wa Tanzanite na kufanikiwa kupata bao la tatu kupitia kwa mchezaji wake Mosili Makhoali dakika ya 61.

Uzoefu wa Afrika Kusini ulionekana dhahiri kwani waliliandama lango la Tanzanite kila mara lakini golikipa Najiat Abbas alikuweza kupangua mashuti kadhaa na mengine kuishia nje lakini uzembe wa mabeki uliweza kusababisha kufungwa bao la nne dakika ya 78 kupitia kwa Mosil Makhoali.
Akizungumza baada ya mchezo kumalizika, Waziri wa habari, vijana michezo na Utamaduni, Fenella Mukangara aliwataka wachezaji kutolia kwani mwanamke jasiri anapanga nini afanye baada ya alichotangulia kukifanya hivyo kwa pamoja na benchi la ufundi wakae watathimini walipokosea ili wafanye marekebisho kwa ajili ya mchezo wa marudiano.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments