KITWANA MANARA, KHALEED ABEID KUONYESHA MAKALI YA ENZI ZAO "Chalenji''
Golikipa Mahiri wazamani wa timu ya taifa Tanzania All Stars Kitwana Manara, pichani (kulia juu).
*******************************
Na Mwandishi wetu
Timu
inayoundwa na wachezaji wa zamani wa timu Taifa ya Tanzania “Tanzania
All Stars” na wale wa Kenya “Wazee wa Kazi” wataonyeshana kazi mjini
Nairobi, Kenya siku ya fainali ya michuano ya Kombe la Chalenji Desemba
12, 2013.
Nyota
wa zamani wa timu ya Yanga na ya Taifa, Kitwana “ Popat” Manara alisema
jana kuwa mechi hiyo ya kihistoria imebalikiwa na Baraza la Vyama la
Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) na wameanza mazoezi makali chini ya
usimamizi wake. Timu hiyo inatarajiwa kuondoka jijini Desemba 10.
Mbali
ya Manara, mchezaji wa zamani wa Simba na timu ya Taifa, Talib Hilal
naye anasimamia mazoezi ya timu hiyo yanayofanyika kila siku jioni
kwenye viwanja vya Leaders Club jijini. Manara alisema kuwa wapo katika
mazoezi ya kina kwa ajili ya mechi hiyo ambayo itachezwa kabla ya
fainali ya mashindano hayo.
Alisema
kuwa wachezaji wote wapo vizuri na malengo yao ni kuonyesha ubora na
vipaji vilivyotukuka walivyokuwa enzi ya ujana wao na kuleta sifa kubwa
katika soka laTanzania. Mbali ya Manara, wachezaji wengine wanaounda
timu hiyo ni Isihaka Hassan, Mohamed Mkweche, Lawrence Mwalusako, David
Mwakalebela, John Mwansasu, Ali Yusuph Tigana, Sekilojo Chambua na
Rashid Idd Chama.
Wengine
ni Edibily Lunyamila, Mohamed Hussein Mmachinga, Khaleed Abeid, James
Kisaka, Omari Gumbo. Kutoka Zanzibar ni golikipa Gopi na Mwinyi Bwanga.
Alisema kuwa wanatarajia kumjumuisha kipa nyota wa zamani, Juma “Mensah”
Pondamali ambaye kwa sasa yupo na timu ya Taifa ya Tanzania, Kilimajaro
Stars inayoshiriki mashindano hayo. Kwa upande wa viongozi ni Hassan
Mnyenye na mjumbe wa Baraza la Michezo nchini (BMT), Jamal Lwambo.
“Lengo
letu ni kuwa na wachezaji wengi zaidi, lakini wengi wao wameshindwa
kujiunga na sisi kutokana na matatizo mbali mbali, hao ndiyo walioitikia
wito huo na wameanza mazoezi, tunaomba wadhamini mbali mbali kutusaidia
ili kuweza kufanikisha safari hiyo, ni gharama kubwa sana na lengo letu
ni kuhamasisha mchezo wa soka, ” alisema Manara.
Huku
timu ya Tanzania ikisaka wadhamini, wenzao wa Kenya wanaendelea na
mazoezi na wamekwisha taja kikosi kitakacho ikabili timu hiyo. Kikosi
hicho kipo chini ya kocha George Sunguti kina wachezaji 30 ambao
waliwika Harambee Stars enzi zao.
Wachezaji
hao ni makipa James Siang’a, Mohammed Abbas, John Busolo huku mabeki
ni , Josphat Murila, Elly Adero, Sammy Pamzo Omollo, Thobias Jua Kali
Ochola, Ben Oloo, George Onyango, Wycliffe Anyangu, Paul Ochieng na John
Bobby Ogola.
Viungo
ni Allan Thigo, Paul Onyiera, ambapo washambuliaji ni Joe Kadenge ,
Peter Dawo , Ben Musuku, Aggrey Lukoye, J.J Masiga , Mike Amwayi,
Douglas Matual, Joe Birgen, Abdul Baraza, Ricky Solomon, James Nandwa, Ambrose Golden Boy Ayoyi, John Nyawaya, David Ochieng’, George Sunguti na Austin Oduor.
Category: tanzania
0 comments