KIBABU FEGY AANIKA KOSA KUBWA ANALOLIJUTIA KULIFANYA MAN U
KOCHA
Sir Alex Ferguson amesema kwamba kosa kubwa alilowahi kufanya wakati
akiwa kazini ni kumuacha beki Mholanzi, Jaap Stam aondoke Manchester
United mwaka 2001.
Kisiki kweli: Stam alipasua alipoondoka United kwa kusema Ferguson alilazimisha aondoke Old Trafford |
Fergusona akiri kosa kumuuza Stam
Beki huyo wa nguvu wa kati alikuwa kisiki cha safu ya ulinzi ya United tangu alipowasili mwaka 1998, lakini akauzwa Lazio kwa dau la Pauni Milioni 15.3 akiwa ana umri wa miaka 29 baada ya kupona majeruhi.
Stam
alielezea katika kitabu chake kwamba Ferguson alilazimisha kuhamia
kwake timu hiy ya Serie A kutokana na mazungumzo yaliyofanyika katika
gari lake kituo cha petroli.Beki huyo wa nguvu wa kati alikuwa kisiki cha safu ya ulinzi ya United tangu alipowasili mwaka 1998, lakini akauzwa Lazio kwa dau la Pauni Milioni 15.3 akiwa ana umri wa miaka 29 baada ya kupona majeruhi.
Akizungumza katika mahojiano ya awali kabla ya mahojiano maalum na Televisheni ya klabu hiyo, MUTV, Ferguson alisema; "Wakati napofikiria maumivu, wazi Jaap Stam wakati wote ilikuwa ni maumivu kwangu, nilifanya maamuzi mabovu wakati huo,".
Uamuzi
mbovu wa Mscotland huyo inasemekana ulitokana na mambo binafasi zaidi,
baada ya kutofautiana na beki huyo kila mtu akiwa kwenye gari lake
wakitoka mazoezini na kumuamuru ajiunge na Lazio haraka iwezekanvyo.
Alitolewa kafara: Mholanzi huyu alitimkia Lazio
Mafanikio: Stam alishinda mataji matatu ya Ligi Kuu England wakati wake akiwa Manchester
Category: uingereza
0 comments