WENGER AFARIJIKA…GIROUD ALIYEUMIA MECHI YA SUNDERLAND JUMAMOSI, YUKO FITI KUCHEZA JUMATANO UFARANSA!!

Unknown | 9:03 PM | 0 comments

Assist master: But he says his job is made easier by players such as Mesut Ozil (right) setting him up


Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
MSHAMBULIAJI wa Asernal,  Olivier Giroud amepunguza hofu juu ya majeruhi aliyoyapata juzi katika mchezo dhidi ya  Sunderland.
Nyota huyo alitolewa nje dakika za mwisho na kocha  Arsene Wenger alikiri kuwa na wasiwasi ya kumkosa mshambuliaji wake pekee ambaye yuko fiti katika kikosi chake.
Lakini mkali huyo raia wa Ufaransa ambaye amefunga kila mchezo wa ligi kuu msimu huu amesema kuwa anaweza kuwa fiti katika mchezo  muhimu wa ufunguzi wa hatua ya makundi wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Marseille jumatano.
I'm ok: There were fears that the injury Olivier Giroud picked up at Sunderland would sideline him
Niko fiti: Kulikuwa na wasiwasi kuwa majeruhi aliyoyapa  Olivier Giroud katika mchezo dhidi ya Sunderland yangemweka nje ya uwanja jumatano ya wiki hii
 
Lack of depth: Arsene Wenger was worried he would be out of strikers for the game on Wednesday
Hali mbaya: Arsene Wenger alikuwa na shaka kuwa atamkosa mshambuliaji wake pekee katika mchezo wa keshokutwa jumatano

Santi Cazorla anatakiwa kuwa nje hadi katikati ya Oktoba na alipoulizwa juu ya maumivu yake, Giroud alisema: “Si mbaya hakika, si mbaya kama nilivyohofia awali. Nilipata pigo mapema mchezoni, lakini hakuna aliyekuwa karibu yangu wakati naumia wakati huo,”alisema.
“Nilikuwa nawania mpira nikadondokea mguu. Nikaumia kifundo cha mguu, lakini bahati nzuri, hakuna maumivu makubwa. Nipo vizuri, kweli nitakuwa safi (kwa mechi na Marseille),”.
Giroud anatakiwa kutambua ukweli kwamba alisajiliwa baada ya kuondoka kwa Robin van Persie Emirates msimu uliopita, na kiwango chake kinaenda kikikua tangu msimu uliopita.
Ameanza vizuri msimu huu na kuna matumaini atafanya vizuri zaidi hasa baada ya kusajiliwa kwa kiungo Mjerumani, Mesut Ozil kwa dau la Pauni Milioni 42.5 kutoka Real Madrid.



On fire: Giroud has scored in every Premier League game this season
Yuko kwenye kiwango: Giroud amefunga katika kila mchezo wa ligi kuu msimu huu
 
Assist master: But he says his job is made easier by players such as Mesut Ozil (right) setting him up
Msaidizi wa nguvu: Lakini amesema kazi yake imekuwa nyepesi kwa kucheza na mchezaji kama Mesut Ozil (kulia)

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments