Asilimia 2% ya mashabiki wa Barcelona hawamtaki Messi.
Lionel Messi ni mchezaji wa kipekee hilo halina ubishi,orodha ya
mafanikio aliyopata kwa maana ya mataji aliyotwaa akiwa na timu ya
Barcelona na tuzo binafsi alizotwaa ni ndefu na ya aina yake kwa
mchezaji mmoja na ni vigumu kuwaza kuwa upo uwezekano hata mdogo tu wa
kuwepo kwa mashabiki hasa wa Fc Barcelona ambao hawamkubali mchezaji
huyu.
Ni vigumu kuamini lakini huo ndio ukweli wenyewe kwamba wapo
mashabiki halisi wa Barcelona ambao hawampendi Messi na wanataka kumuona
akiondoka na kuwaachia timu yao .
Hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotoka kwa Rais wa Barcelona Sandro
Rossel ambaye amefichua kwamba matokeo ya kura ya ndani kwa ndani
iliyoendeshwa miongoni mwa mashabiki wa Barcelona ambayo imeonyesha kuwa
asilimia mbili ya mashabiki wote wa Barcelona hawamtaki Lionel Messi .
Rossel amesema kuwa ameshangazwa na hakutegemea kama angekuwepo mtu
anayejiita shabiki wa Barcelona mwenye uthubutu wa kusema hataki kumuona
Messi akiwa sehemu ya Barcelona na angependa kuwafahamu mashabiki hao
ikiwezekana hata kukutana nao na kuwahoji ili wampe sababu za kutompenda
Messi .
Pamoja na hayo asilimia 98% ya mashabiki iliyobakia bado wanampenda
Messi ambaye ni mchezaji Muhimu pengine kuliko wote ndani ya Barcelona .
Category: uingereza