PSG wabeba Kombe Ufaransa

Unknown | 5:34 PM | 0 comments

Lyon, Ufaransa .Paris St-Germain imetwaa Kombe la Ufaransa kwa mara ya nne mfululizo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Monaco kwenye Uwanja wa Lumieres mjini Lyon.

Bao la Julian Draxler dakika ya nne liliipa PSG uongozi licha ya kuwa aliotea, lakini Monaco walisawazisha kupitia kwa mkwaju wa Thomas Lemar wa umbali wa mita 20.

Angel Di Maria aliipa tena PSG uongozi kwa bao la pili kabla ya matumaini ya Monaco kutwaa taji kubwa tangu 2003 kufutika kwa mabao mawili ya mwisho ya Edinson Cavani ya kipindi cha pili.

Cavani aliunganisha vizuri kwa shuti hafifu mpira mrefu kuandika bao la tatu na kufanya mchezo kuwa mgumu zaidi kwa Monaco.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uruguay, alimchungulia kipa wa Monaco, Danijel Subasic na kufunga kwa shuti la kiufundi bao la nne akibinuka huku akilipa mgongo lango la Monaco.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments