Samattah awapa neno zito Yanga na Azam
Kuelekea michezo ya kimataifa ya vilabu bingwa Afrika pamoja na Confederation Cup, Mbwana Samatta amevitakia kila la heri vilabu vya Yanga na Azam ambavyo vinaipeperusha bendera ya Tanzania kwenye michuano hiyo katika msimu huu.
“Mimi nawatakia kila la heri Yanga pamoja na Azam kwa sababu wanawakilisha nchi na mimi ni mtanzania pia.”
“Nawaombea kwa Mungu waweze kushinda kwenye hizo game na wasonge mbele, kwa sababu wanaposhinda na kusonga mbele maana yake bendera inazidi kusonga mbele na ni maendeleo kwa sababu ukiangalia hata kwenye viwango vya FIFA, tuko mbali tumepitwa na Kenya na Uganda lakini naamini Tanzania ina vipaji vingi kuliko hizo nchi nilizozitaja.”
“Kwa hiyo timu kama hizo zinapokuwa zinafanya vizuri katika mashindano ya kimataifa, maana yake zinasukuma bendera na kupandisha nchi yetu kwenye viwango vya FIFA taratibu na mwisho wa siku tutafika kule tunapopataka.”
Yanga inacheza na Zanaco leo Jumamosi March 11, 2017 ikiwa ni wawakilishi wa miachuano ya mabingwa Afrika kwenye uwanja wa taifa wakati Azam wao watacheza kesho Jumapili March 12, 2017 dhidi ya Mbabane Swalows kwenye uwanja wa Azam Complex, Chama
Category: uingereza
0 comments