Hii ndio ratiba ya kufuzu kombe la Dunia 2018 Bara la Ulaya

Unknown | 4:06 PM | 0 comments

Ijumaa hii ya Machi 24 kutakuwa na mechi katika bara la Ulaya za kuwania kufuzu kombe la dunia mwakani nchini Urusi.

Mechi hizo zitakazochezwa ni pamoja na michezo ya kundi D, ambapo Georgia watacheza na Serbia, Austria watakua wenyeji wa Moldova na Ireland wakicheza dhidi ya Wales.

Katika kundi G Hispania watakipiga na Israel, Liechtenstein wao watapimana ubavu na Macedonia, timu ya taifa ya Italia itacheza dhidi ya Albania.

Wakati huo huo Croatia wao watakua wenyeji wa Ukraine, huku Kosovo wakicheza na Iceland na Finland watakuwa ugenini dhidi ya Uturuki hii ikiwa ni michezo ya kundi I.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments