Yanga yaibomoa Ndanda

Unknown | 8:41 PM | 0 comments

Kelele na tambo za Ndanda FC ya Mtwara kwamba ingeweza kuibuka na ushindi leo zimezimwa kwa kufungwa bao 4-0 na wenyeji wao mabingwa watetezi wa taji la ligi kuu Tanzania bara Yanga.


Mchezo huo uliopigwa katika dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam ulikua muhimu kwa Yanga kushinda ili kuwapoza mashabiki wao baada ya kutoka Sare katika mechi iliyopita dhidi ya African Lyon.

Mshambuliaji Donald Ngoma akirejea kutoka katika majeraha aliwaweka Yanga mbele mapema mnamo dakika ya 4 ya mchezo kwa bao zuri la kichwa akiunganisha mpira wa kona wa Haruna Niyonzima,Ngoma alirudi tena katika dakika ya 21 kwa bao la pili  kabla ya Amisi Tambwe kufunga bao la tatu dakika ya 25 na kuifanya Yanga kwenda mapumziko Ikiwa mbele kwa mabao 3-0.
Kipindi cha pili Ndanda FC walizinduka lakini juhudi zao hazikufua dafu katika beki ya Yanga iliyokua Ikiongozwa na Vicent Bossou na Calvin Yondani.

Kipindi cha pili kilitawaliwa zaidi na Yanga huku, golikipa wa Ndanda Jeremia Kisubi akiokoa michomo mingi iliyoelekezwa langoni mwake.
Mnamo dakika ya 89. Vicent Bossou aliiandikia Yanga bao la nne kwa kichwa na kuhitimisha karamu ya mabao manne katika mchezo huo.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments