Real Madrid yatwaa Ubingwa wa Dunia

Unknown | 10:44 AM | 0 comments


Mabingwa wa Ulaya Real Madrid jana waliweza kumaliza mwaka kwa kuongeza ubingwa wa Klabu duniani kwa kuifunga Kashima Antlers ya Japan kwa bao 4-2.

Katika mchezo huo Cristiano Ronaldo aligunga mabao matatu peke yake mchezo ambao ilibidi uende mpaka dakika 120 baada kukosekana mshindi ndani ya dakika 90 matokeo yakiwa ni sare ya bao 2-2.

Huko England Wenyeji Manchester City waliifunga Arsenal bao 2-1 mabao ya Leroy Sane na Raheem Sterling huku Tottenham ikiibuka na ushindi kama huo dhidi ya Burnley magoli ya Delle Alli na beki Danny Rose.

Nchini Spain mabingwa watetezi Barcelona waliweza kuinyuka Espanyol bao 4-1 mshambuliaji Luis Suarez akifunga mabao mawili huku Lionel Messi na beki Jordi Alba wakifunga bao moja kila mmoja.

Nchini Ufaransa Monaco walipunguzwa kasi na Lyon kwa kufungwa bao 3-1 katika mwendelezo wa ligi kuu ya Ufaransa League One ambayo Ilishuhudia pia ikishinda bao 2-1 magoli ya Mario Ballotel na kuzidi kuipaisha timu hiyo katika nafasi ya kwanza.

www.wspendasoka.com tumekuwekea hapa matokeo yote ya mechi za jana kwa kifupi pamoja na ratiba ya mechi za leo kwa muda wa Afrika Mashariki.

FIFA Club World Cup

Real Madrid 4-2 Kashima Antlers

English Premier League

AFC Bournemouth 1-3 Southampton
Manchester City 2-1 Arsenal
Tottenham Hotspur 2-1 Burnley

Spanish Primera División

Leganes 1-1 Eibar
Deportivo La Coruña 2-0 Osasuna
Barcelona 4-1 Espanyol

German Bundesliga

SV Darmstadt 98 0-1 Bayern Munich
Bayer Leverkusen 1-2 FC Ingolstadt 04

Italian Serie A

Sassuolo 0-1 Internazionale
Chievo Verona 2-1 Sampdoria
Napoli 5-3 Torino
Udinese 2-0 Crotone
US Pescara 0-3 Bologna
Genoa 3-4 Palermo
Lazio 3-1 Fiorentina

French Ligue 1

Caen 3-0 Metz
Nice 2-1 Dijon FCO
Marseille 2-0 Lille
AS Monaco 1-3 Lyon

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments