TP Mazembe mabingwa Afrika

Unknown | 8:18 PM | 0 comments

Lubumbashi, DR Congo. Kiungo Mzambia Rainford Kalaba alikuwa shujaa wa TP Mazembe ya DR Congo baada ya kuiongoza kuirarua Mouloudia Bejaia ya Algeria kwa mabao 4-1 katika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Huo ni ushindi wa kwanza kwa mabingwa hao ambao katika mchezo wa kwanza walitoka sare ya 1-1 nchini Algeria.

Kwa matokeo hayo, Mazembe imetwaa ubingwa kwa mabao 5-2 na kuondoka na kitita cha Dola 660,000 na MO Bejaia Dola 462,000.

Mabao ya Merveille Bope, Kalaba (mawili), Jonathan Bolingi yalitosha kuipa ushindi klabu hiyo ambao MO Bejaia walijifuta machozi kwa bao dakika ya 75 la Sofiane Khadir.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments