Tathmini na matokeo ya mechi za jana Za EPL
Raundi ya 12 ya ligi kuu nchini England iliendelea Jumamosi hii kwa michezo 8 kuchezwa huku magoli 19 yakifungwa katika michezo hiyo.
Pambano lililokua likiangaliwa sana na mashabiki wengi wa soka ni lile lililowakutanisha Arsenal ambao walisafiri kuwavaa Manchester United katika dimba la Old Trafford.
Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya bao 1-1 Juan Mata akitangulia kufunga bao kabla ya Olivier Giroud hajaisawazishia Arsenal dakika za lala salama.
Mchezo huo ambao ulitawaliwa sana na viungo wa kati ulianza kwa kasi na Arsenal wakionekana kuumiliki vyema mchezo huo licha ya kushindwa kupiga mpira wowote langoni mwa United mpaka pale Olivier Giroud alipofunga bao pekee akiunganisha mpira wa krosi wa Alex Oxilade-Chamerlain.
Manchester United walionekana kuimarika hasa kwa nafasi ya kiungo ambapo mkongwe Michael Carick aliendelea kuwa kumuaminisha kocha Jose Mourinho kama anaweza huku zikitengenezwa nafasi kadhaa za kufunga lakini washambuliaji hawakuweza kuzifanyia kazi mpaka Juan Mata alipoweza kufunga bao pekee akiunganisha mpira wa krosi ya Ander Hererra.
CRYSTAL PALACE 1-2 MAN CITY
Yaya Toure aliitwa kwa mara ya kwanza na kocha Pep Guadiola kuanza katika mchezo huo na Yaya hakufanya ajizi alitumia vyema nafasi hiyo kwa kufunga magoli yote mawili yaliyowapa ushindi Manchester CitySOUTHAMPTON 0-0 LIVERPOOL
Licha ya kocha Juggen Klopp kuendelea kuwatumia washambuliaji wake watatu katika safu ya Ushambuliaji yani Sadio Mane,Philip Coutinho na Firmino alishindwa kabisa kuipenya ngome ya Southampton na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare hiyo tasa.
SUNDERLAND 3-0 HULL CITY
Sunderland waliendelea kuzinduka wakipata ushindi wao wa pili katika ligi ukiwa ni ushindi wa pili mfululizo na kufikisha pointi 8 katika nafasi ya 19.Magoli mawili ya Victor Anichebe na moja la Jermain Defoe yalitosha kuendelea kusogeza siku kwa kocha David Moyes wa Sunderland.
TOTTENHAM 3-2 WEST HAM
Pambano la mwisho Jumamosi lilikua kati ya Tottenham Hotspur dhidi ya West Ham katika dimba la White Hart Lane jijini London ambapo Tottenham iliendeleza matokeo mazuri msimu huu kwa kuibuka na ushindi huo ikiwa ni timu pekee ambayo haijapoteza mchezo wowote mpaka sasa.Harry Kane baada ya majeruhi ya Muda mrefu alirejea na kufunga magoli mawili kati ya magoli matatu lingine likifungwa na Harry Winks huku West Ham ambao walionesha kila nia ya kuibuka na ushindi wakipata magoli yao kupitia kwa Antonio na Lanzini.
WATFORD 2-1 LEICESTER CITY
Mabingwa watetezi Leicester City waliendeleza matokeo mabaya kwa kufungwa bao 2-1 na Watford hali iliyozidisha ugumu kwa mabingwa hao.STOKE CITY 0-1 BOURNEMOUTH
Stoke City wakiwa nyumbani walilambwa bao 1-0 na Bournmeouth kwa goli pekee la Nathani Ake huku Bojan Kirkic akikosa penati kwa upande wa Stoke City.
EVERTON 1-1 SWANSEA
Kocha mpya wa Swnsea Mmarekani Bob Bradley alipata pointi moja ugenini dhidi ya Everton katika mechi ambayo Swansea waliongoza kwa muda mrefu baada ya kupata goli la kipindi cha kwanza la Gyfil Sidgusson kabla Everton hawajasawazisha dakika za lala Salama kupitia kwa Coleman.
Ni hayo tu yaliyojiri kwa Jumamosi Jumapili ni Chelsea dhidi ya Middlesbrough.
Category: uingereza
0 comments