Simba, Yanga kukipiga leo

Unknown | 1:48 PM | 0 comments

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inaendelea leo kwa viwanja sita ambako kwa mara ya kwanza timu zote za Dar es Salaam zitakuwa mikoani kupambana kutafuta nafasi bora katika ligi hiyo iliyoanza Agosti 20, 2016 kabla kufifikia ukomo wa mzunguko wa 15, Novemba 12, mwaka huu.

Vinara ligi hiyo kwenye msimamo msimu wa 2016/17, Simba SC watakuwa wageni wa Stand United kwenye Uwanja wa CCM Kambarage wakati mabingwa watetezi wa taji hilo Young Africans itakaribishwa na Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Africans Lyon pia ya Dar es Salaam itakuwa mkoani Pwani kucheza na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani wakati Maafande wengine kutokea mkoani humo – JKT Ruvu watakuwa wageni wa Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Majimaji ilihali Ndanda itawakabiri Ndanda FC kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara huku Toto African ikiwakaribisha Azam kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Wakati ligi hii ikiingia ukiongoni kwa nusu msimu, TFF inatoa wito kwa timu kuajiandaa na dirisha dogo la usajili linalotarajiwa kuanza Novemba 15, mwaka huu kusajili wachezaji mahiri ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mwendelezo wa ligi hiyo nusu ya msimu uliobaki utakaoanza baadaye Desemba.
Wakati wa usajili wa dirisha dogo ndipo michuano ya hatua ya awali ya kuwania Kombe la Shirikisho la Azam 2016/2017 inatarajiwa kuanza Novemba 19, mwaka huu ambako pia imepangwa kuzindua michuano hiyo huko mkoani Mara.

Safari hii timu shiriki zimeongezwa mabingwa wa mikoa wa mwaka jana hivyo kufikisha idadi itakayofika 86 badala ya 64 za msimu ulioipita. Imechukuliwa mikoa 22 baada ya ile mitano, kupanda Daraja kucheza Ligi Daraja la Pili msimu huu ambayo imeanza kushika kasi.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments