Yanga hii ni balaa ... Mechi mbili yapiga goli 10

Unknown | 5:05 AM | 0 comments

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka Tanzania bara Yanga imeendeleza kasi yake ya kugawa dozi katika mfululizo wa mechi za ligi hiyo wakiifunga JKT Ruvu kwa bao 4-0.



Ushindi huo umekuja siku chache baada ya mabingwa hao kuikandamiza Kagera Sugar kwa bao 6-2 katika mchezo uliopigwa huko Bukoba katika dimba la Kaitaba na kufikia magoli 10 katika mechi mbili.

Mchezo wa leo dhidi ya JKT Ruvu ulipigwa katika dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam ambapo Yanga iliingia uwanjani ikiwa ni mechi ya kwanza bila ya kocha Hans van der Pluijm aliyeamua kuachana na klabu hiyo.

Mshambuliaji Obrey Chirwa aliendelea  kufunga katika mechi za ligi hiyo akifunga bao la kwanza ambalo lilidumu mpaka mapumziko

Kipindi cha pili Yanga ikiendeleza wimbi la kusaka magoli kwa kuongeza bao la pili lililofungwa na Amiss Tambwe aliyeingia dakika chache kabla ya kufunga bao hilo. Simon Msuva aliongeza bao la tatu kisha Amiss Tambwe akafunga bao la 4 na kufanya mchezo huo kumalizika kwa ushindi huo mnono wa bao 4-0.

Kwa matokeo hayo Yanga imefikisha pointi 24 katika nafasi ya pili ikiwa ni pointi 5 nyuma ya Simba inayoongoza.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments