Stand United yaifukuzia Simba kileleni, Azam fc hoi, Julio anawa mikono

Unknown | 7:41 AM | 0 comments

Stand United maarufu kama Chama la wana toka Shinyanga imeendelea kufanya vizuri katika ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.


Ikicheza ugenini katika dimba la Maji Maji mjini Songea Stand iliibuka na ushindi wa bao 2-0 ikiwafunga wenyeji Maji Maji FC.

Matokeo hayo yanaipandisha Stand United katika msimamo wa ligi kuu Tanzania bara kwa kufikisha pointi 15 katika nafasi ya pili ikiwa ni pointi 2 nyuma ya Vinara wa ligi hiyo Simba SC.

Katika mechi nyingine jana Matajiri Azam FC wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani Azam Complex walishindwa kuibuka na pointi zote 3 na kulazimisha sare ya bao 2-2 dhidi ya Ruvu Shooting.

Azam imeendelea kuwa na matokeo mabaya tangu ilipopoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Simba ikafungwa na Ndanda 2-1 mchezo uliofuatakabla ya na kuambulia sare hiyo ya bao 2-2 ikifikisha pointi 11 katika nafasi ya 5

Huko Jijini Mbeya wenyeji Mbeya City waliinyuka Mwadui FC kwa bao 1-0 mchezo uliolalamikiwa vilivyo na kocha wa Mwadui Jamhuri Kiwelu Julio ambaye ametangaza kubwaga manyanga akisema waamuzi wamekua wakiikandamiza kwa makusudi timu yake.

Mtibwa Sugar toka Mantoka Morogoro wakicheza katika uwanja wao wa nyumbani waliwafunga African Lyon bao 1-0 wakati Kagera Sugar ikitoshana nguvu na Prisons ya Mbeya kwa kwenda sare ya bila kufungana huku Mbao FC ikitoshana nguvu JKT Ruvu kwa sare ya bila magoli pia.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments