Messi apiga hat trick, Arsenal washusha kipigo kitakatifu
LIONEL Messi ameondoka na mpira wake huko Nou Camp baada ya kufunga bao tatu zote kwa mguu wa kushoto wakati Barcelona ilipoichapa Manchester City 4-0 kwenye mechi ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Wakati supastaa huyo wa Argentina akiondoka na zawadi hiyo ya mpira, huko Emirates, vijana wa Arsene Wenger, Arsenal wameshusha kipigo kizito, wakiichapa Lidogorets Razgrad 6-0, huku kiungo fundi wa mpira kutoka Ujerumani, Mesut Ozil akipiga 'hat-trick' katika mchezo huo.
Iliwachukua dakika 12 tu Arsenal kuandika bao la kwanza kupitia kwa Alexis Sanchez, aliyechopu mpira kabla ya Theo Walcott kupiga la pili dakika tatu kabla ya filimbi ya mapumziko. Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na Arsenal iliendelea kugawa dozi kwa wapinzani wao ambapo Alex Oxlade Chamberlain akapiga bao kwenye dakika 46 kabla ya Ozil kutupia mara tatu mfululizo kwenye dakika 56, 83 na 87.
Category: uingereza
0 comments