Yanga yagongwa kimoja na Stand United
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara Yanga wameangua pua baada ya kuchapwa bao 1-0 na Chama la wana Stand United.
Goli pekee la Stand United lilifungwa na Pastory Athanas kipindi cha pili na kuifanya Yanga kupoteza mchezo wake wa kwanza msimu huu katika ligi hiyo kubwa kabisa kwa ngazi ya vilabu hapa Tanzania.
Yanga wanaelekea katika mchezo wao na watani zao Simba hapo Jumamosi mchezo ambao unaonekana utakua mgumu kwa Yanga baada ya watani zao hao kuongoza ligi huku wakiwa na kikosi bora msimu.
Category: tanzania
0 comments