Wanaume kazini wikiendi hii VPL
Raundi ya nne ya ligi kuu soka Tanzania bara inaanza leo kwa mechi 5 kuchezwa katika viwanja tofauti.
Mechi zitakazoonyeshwa na Azam TV |
Huko Mbeya Wenyeji Mbeya City watakua na kazi pevu kuumana na Azam FC ambayo iliitandika Prisons ya huko bao 1-0 katika mchezo uliopigwa Jumatano wiki hii.
Uwanja wa mabatini kule Pwani Ndugu wawili watakua wakiumana Jkt Ruvu watawaalika Ruvu Shooting ambao katikati ya wiki walifungwa bao 2-1 na Simba.
Huko Shinyanga shughuli ni pevu kati ya Mwadui FC watakaokuwa katika dimba lao la Mwadui kuwaalika Wapiga debe Stand United.
Ndanda FC ya Mtwara baada ya kuibania Yanga leo itakua katika uwanja wao huo huo wa Nangwanda kucheza na Kagera Sugar toka Mkoani Kagera.
Category: tanzania
0 comments