Hii hapa ratiba ya soka ligi kuu Tanzania Bara ya leo
Mzunguko wa 6 wa ligi kuu ya soka Tanzania bara unaanza leo kwa viwanja vitano kuwa katika hali ngumu.
Huko Mtwara wenyeji Ndanda FC wataikaribisha Azam FC ambayo tayari iko huko Tangu Alhamisi wakitoka Dar walikopoteza mchezo wao uliopita dhidi ya Simba.
Mwadui FC chini ya kocha mwenye maneno mengi Jamhuri Kiwelu "Julio" watakua wageni wa Prisons ya Mbeya katika dimba la Sokoine jijini Mbeya.
JKT Ruvu wao watakua uwanja wa mabatini kuwaalika Mbeya City ya jijini Mbeya huku Mtibwa Sugar wakiialika Mbao FC ya Mwanza katika dimba la Manungu Complex.
Category: tanzania
0 comments