SIMBA YANG'ANG'ANIWA, AZAM YATAKATA
Wekundu wa Msimbazi Simba leo wameshindwa kuendeleza wimbi lake la ushindi baada ya kukomaliwa na kulazimishwa sare ya bila kufungana na JKT Ruvu.
Safu bora ya ulinzi ya JKT Ruvu ilikua ndiyo kikwazo kwa washambuliaji wa Simba wakiongozwa na Laudit Mavugo na Blagnon badae akaingia Ibrahim Ajib.
Katika mchezo mwingine katika uwanja wa Azam Complex wenyeji Azam FC waliweza kuifunga Maji Maji Ya Songea kwa bao 3-0.
Nahodha John Bocco alifunga bao 2 huku Kiungo Mudathir Yahya akifunga bao 1.
Katika mechi zingine Mwadui iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbao FC huku Mtibwa wakishinda bao 2-1 dhidi ya Ndanda FC.
Category: tanzania
0 comments