SIMBA YAMTAKA KESSY AWALIPE MAMILIONI
kata la mchezaji Hassan Ramadhani Kessy kuidhinishwa kuichezea Yanga limeingia katika sura mpya ambapo klabu yake ya Zamani Ya Simba wamemtaka mchezaji huyo kuwalipa mamilioni ya pesa.
Mapema wiki iliyopita Kamati inayoshughulika na maswala ya wachezaji katika shirikisho hilo walimwidhinisha Kessy kuichezea Yanga huku ikisema kwamba Simba wanaweza kuendelea kumdai mchezaji huyo lakini sio kumzuia kucheza.
Madai ya Simba ni kwamba Kessy alivunja mkataba wao kwa kushiriki shughuli za Yanga huku akijua kwamba bado ana mkataba na Simba.
Category: tanzania
0 comments