STAA WA SIMBA ASAINI KUJIUNGA NA YANGA
Baada ya headlines za muda mrefu kuhusishwa kutaka kuhama klabu ya Simba na kuhitajika na watani wa jadi wa Simba klabu ya Dar es Salaam Young Africans, hatimae leo May 9 2016 ushaidi wa picha umewekwa wazi baada ya beki Hassan Kessy kusaini mkataba wa miaka miwili na klabu ya Simba.
Kuanzia kushoto ni Kaimu katibu mkuu wa Yanga Baraka, Hassan Kessy na meneja wa mchezaji huyo Athumani Tippo
Kessy ambaye awali aliripotiwa kuwa na mgogoro na klabu ya Simba hususani baada ya kumchezea faulo mchezaji wa Toto Africans Christopher Edward alionyeshwa kadi nyekundu na siku tatu baadae Simba wakatangaza kumfungia mechi tano kutokana na kosa hilo lakini mkataba wake Simba ulikuwa unaisha
Category: tanzania
0 comments