MAN UNITED YAUA 3-1 NA KUFUZU EUROPA LEAGUE
TIMU ya Manchester United imefanikiwa kukata tiketi ya kucheza michuano ya Europa League baada ya ushindi wa mabao 3-1 usiku huu dhidi ya Bournemouth katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
Mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Old Trafford leo, ilikuwa ufanyike juzi lakini ukaahirishwa kutokana na hofu kutegwa kwenye Uwanja huo.
Nahodha Wayne Rooney aliifungia United bao la kwanza akimalizia krosi ya Anthony Martial dakika ya , hilo likiwa bao lake la 100 kufunga Uwanja wa Old Trafford.
Category: uingereza
0 comments