Louis van Gaal kasema yeye ni moja ya makocha bora duniani, hizi ndio comment alizokutana nazo
Kocha wa klabu ya Man United ya Uingereza Louis van Gaal huenda ndio akawa kocha ambaye yupo katika wakati mgumu kwa sasa kuliko kocha yoyote Uingereza, Louis van Gaal ameongea kauli ambayo imemfanya akumbane na comment nyingi.
Van Gaal amenukuliwa
akisema kuwa yeye ni moja kati ya makocha bora duniani, kitu ambacho
kimemfanya akumbane na comment nyingi za kumkosoa kutokana na klabu yake
ya Man United ipo katika nafasi ya 5 tofauti na ilivyozoeleka kuwa klabu hiyo huwa katika nafasi tatu hadi nne za juu.
Kwa sasa Van Gaal ambaye alisema “mimi ni moja kati ya makocha bora duniani” anaripotiwa kuwa nafasi yake mwisho wa msimu itarithiwa na kocha wa zamani wa Chelsea Jose Mourinho, hivyo kauli ya yeye kujiita bora haikuwapendeza mashabiki wa soka hususani watumiaji wa mtandao wa twitter.
Category: uingereza
0 comments