YANGA YAENDELEA KUGAWA DOZI NENE

Unknown | 7:18 AM | 0 comments

YANGA SC imetinga Robo Fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation baada ya kuifunga JKT Mlale mabao 3-1 jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mlale JKT ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao jioni ya leo kupitia kwa Shaaban Mgandila dakika ya 21 akimalizia krosi maridadi ya Edward Songo.
Yanga SC ilifanikiwa kupata bao la kusawazisha kupitia kwa mshambuliaji wake, Paul Nonga dakika ya 38 aliyemalizia pasi ya winga Godfrey Mwashiuya.

Thabani Kamusoko (kushoto) ameifungia bao ushindi Yanga leo

Yanga SC walipata bao la ushindi dakika ya 58 kupitia kwa kiungo wake Mzimbabwe, Thabani Kamusoko aliyemalizia tena krosi ya winga machachari, Mwashiuya.
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’ Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Said Juma ‘Makapu’, Simon Msuva, Salum Telela/Thabani Kamusoko dk54, Matheo Anthony/Donald Ngoma dk46, Paul Nonga/Malimi Busungu dk59 na Godfrey Mwashiuya. 
JKT Mlale; Noel Murish, Lucas Chapanga, Gerimanius Chindera, Said Ngapa, Frank Tesha, Othman Mhagama, Shaaban Mgandila, Omar Mnubi, Richard Mwadiga, Edward Songo na Alex Sethi/Raphael Siame dk50.  BIN ZUBERY

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments