THOMAS ULIMWENGU AWEKA REKODI MPYA

Unknown | 12:45 PM | 0 comments

TP Mazembe imechukua kwa mara ya tatu African Super Cup baada ya kuifunga Tunisian Red Devils “Etoile Du Sahel” kwa magoli 2-1.

TP Mazembe imepata ushindi kutokana na magoli ya striker wa Ghana Daniel Nii Adjei ambae alitupia goli la kwanza dakika ya 20 na 45.

Mechi hiyo iliisha kwa kushuhudia goli moja la pekee kwa upande wa Etoile Du Sahel kutoka kwa Mohamed Msekh.

Mtanzania Thomas Ulimwengu amekua mchezaji kwanza kutoka Tanzania kushinda kombe hili baada ya mechi ya leo.

Thomas aliingia dakika ya 73, kwa mujibu wa taarifa ni kwamba kocha hakuweza kumchezesha muda mrefu kwasababu ana maumivu ya kifundo cha mguu alipata kwenye mechi dhidi ya Lupopo. Kuna uwezekano akapewa wiki nzima kupumzika ili apone vizuri.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments