MAN UNITED, LIVERPOOL NA SPURS ZAZIDI KUCHANJA MBUGA EUROPA LEAGUE
MANCHESTER United, Liverpool na Tottenham Hotspur zote zimekwenda hatua ya 16 Bora Kombe la UEFA Europa League, baada ya ushindi wa mechi za marudiano leo.
Manchester United imeichapa mabao 5-1 FC Midtjylland usiku huu Uwanja wa Old Trafford na kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 6-3.
Wakiwa wanaongoza kwa ushindi wa 2-1 kwenye mchezo wa nyumbani, Midtjylland walitangulia kupata bao kupitia kwa Pione Sisto dakika ya 27, kabla ya Nikolay Bodurov kujifunga dakika ya 32 kuisawazishia United.
Marcus Rashford akafunga mara mbili mfululizo dakika ya 63 na 75, kabla ya Ander Herrera kufunga kwa penalti dakika ya 87 na Memphis Depay kuhitimisha ushindi wa wenyeji kwa bao la tano dakika ya 90.
Bao pekee la James Milner kwa penalti dakika ya tano, limetosha kuipa ushindi wa 1-0 Liverpool dhidi ya FC Augsburg Uwanja wa Anfield na kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 1-0 baada ya sare ya 0-0 kwenye mchezo wa kwanza.
Tottenham Hotspur imeitandika 3-0 Fiorentina, mabao ya Ryan Mason dakika ya 25, Erik Lamela dakika ya 63 na Gonzalo Rodriguez aliyejifunga dakika ya 81 Uwanja wa White Hart Lane na kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-1 baada ya sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza.
Ryan Mason akishangilia baada ya kuifungia Tottenham na kuipa tiketi ya hatua ya 16 Bora michuano ya Europa League PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Michezo mingine, bao la kujifunga la kipa Iker Casillas dakika ya 23 limewapa ushindi wa 1-0 wageni Borussia Dortmund dakika ya 23 Uwanja wa Estadio do Dragao. Dortmund inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-0, baada ya awali kushinda 2-0 nyumbani.
Bao pekee la Eirik Hestad dakika ya 43 limetosha kuipa ushindi wa 1-0 Molde 1-0, Uwanja wa Aker Stadion na hivyo kusonga mbela kwa ushindi wa jumla 3-1 baada ya awali kushinda 2-0 nyumbani.
Napoli imetoa sare ya 1-1 na Villarreal, FC Basel imeifunga 2 - 1 St Etienne, Lazio imeifunga 3-1 Galatasaray, Valencia CF.
James Milner (katikati) cakishangilia baada ya kufungia Liverpool kwa penalti PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Category: uingereza
0 comments