Azam FC wamefunga usajili wao kwa kunasa saini ya staa huyu ….
Headlines za usajili zinazidi kuchukua
nafasi kwa mwezi November hususani katika kipindi hiki cha usajili cha
dirisha dogo, ikiwa zimesalia sio zaidi ya siku 15 ili iweze kufikia
December 15 dirisha dogo la usajili kwa Ligi Kuu soka Tanzania lifungwe, uongozi wa klabu ya Azam FC umethibitisha rasmi kumsajili golikipa mkongwe aliyeachwa na Simba Ivo Mapunda.
November 30 Afisa mtendaji mkuu wa klabu ya Azam FC Saad Kawemba amethibitisha kusajiliwa kwa Ivo Mapunda, baada ya kufanya mazoezi na klabu yao kwa kipindi cha miezi mitatu na kocha wao muingereza Stewart Hall kuvutiwa na nidhamu na uwezo wa golikipa huyo.
“Ivo
aliomba kufanya mazoezi na Azam FC ili ajiweke sawa na kocha alikubali
lakini nidhamu yake, uwezo wake na ushirikiano wake na wachezaji wenzake
umemvutia kocha, hivyo kocha akaomba aongezewe golikipa wa tatu mwenye
uzoefu, ndio tukamsajili Ivo ambaye mkataba wake hauzidi mwaka kwani ana
mipango yake na sasa tumefunga usajili wa dirisha dogo” >>> Saad Kawemba
Kufuatia kusajiliwa kwa Ivo Mapunda, Azam FC inakuwa na magolikipa watatu Aishi Manula, Mwadini Aly na Ivo Mapunda aliyejiunga rasmi wiki hii. Ivo Mapunda aliachwa na Simba mwanzoni mwa msimu huu wa Ligi Kuu soka Tanzania bara baada ya uongozi wa klabu Simba kuridhia kuwaacha wachezaji wawili Ivo pamoja na mshambuliaji wa Stand United Elias Maguli, hivyo Maguli aliwahi kupata timu mapema ila Ivo alikuwa nje ya uwanja.
Category: tanzania