ASAMOAH GYAN KULIPWA MSHAHARA WA ZAIDI YA £163,000 KWA WIKI
Mpira ni
pesa, hakuna fujo wala figisufigisu. Mchezaji wa Ghana ambae aliwai
kucheza kwenye Sunderland kwenye ligi ya uingereza anaendelea kupiga
pesa nyingi baada ya kuhama kwenye club za ulaya.
Hivi sasa
anahama kutoka club ya Al Ain ambayo makazi yake yapo Abu Dhabi na
kujiunga na club ya Shanghai SIPG. Asamoah ameonekana akiwasili kwenye
uwanja wa ndege wa Shanghai akienda kwenye kazi moja tu ambayo ni
kusaini mkataba na club hiyo ambayo inafundishwa na kocha Sven-Goran
Eriksson.
Asamoh
anatarajia kulipwa mshahara mkubwa zaidi ya ule ambao alikua analipwa na
Al Ain ambapo alikua analipwa £163,000. Mchezaji huyu mwenye miaka 29
amepokelewa na mashabiki wengi akitegemea kushiriki Chinese Super
League.
Club ya
Shanghai SIPG inasajili majina makubwa kwa lengo la kupata ushindi
kwenye mechi na pia kupata umaarufu ambao wataumia kuiuza brand ya club
yao kwenye makapuni mengi ya kibiashara yalipo China. Fursa ya biashara
nchini China ni kubwa na ushabiki wa soka upo juu, ndio maana hawasiti
kuwekeza pesa za kutosha ili kuzikuza club zao.
Category: uingereza
0 comments