MESSI AFIKIA REKODI YA MAGOLI YA KUFUNGA KWENYE UEFA CHAMPIONS LEAGUE
Mshambuliaji
kutoka nchini Argentina na klabu ya Barcelona Lionel Andrés "Leo" Messi
Cuccittini amekuwa wa kwanza kuifikia rekodi ya ufungaji mabao mengi
kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, iliyokuwa inashikiliwa
na aliyekua mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid pamoja na Schalke 04
ya nchini Ujerumani Raúl González Blanco.
Messi
ameifikia rekodi hiyo usiku wa kuamkia hii leo baada ya kuifungia
Barcelona mabao mawili katika mchezo wa mzunguuko wa nne wa michuano ya
ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Ajax Amsterdam uliochezwa huko
Amsterdam Arena.
Kabla
ya mchezo huo Messi alikua ameshafunga idadi ya mabao 69 katika
michuano hiyo mikubwa barani Ulaya upande wa vilabu na alikua akihitaji
mabao mawili ili kuifikia rekodi ya mabao 71 ambayo iliwekwa na Raul
akiwa na klabu ya Schalke msimu wa 2010–11.
Hata
hivyo Messi amefikisha idadi hiyo ya mabao baada ya kucheza michezo 90
ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, ikiwa ni tofauti kubwa na Raul ambaye
alifikisha mabao 71 baada ya kucheza michezo 144, huku Cristiano Ronaldo
mwenye mabao 70 ameshacheza michezo 107.
Messi pia
ameweka rekodi ya kufikia rekodi hiyo akiwa na umri mdogo wa miaka 27
tofauti na wapinzani wake ambapo Rul aliweka rekodi hiyo akiwa na umri
wa miaka 34 na aneyemfuatia kwa sasa Ronaldo ana umri wa miaka 29.
Category: uingereza
0 comments