REAL MADRID YALAZIMISHWA 1-1 NA ATLETICO SUPER CUP YA KWANZA BERNABEU

Unknown | 9:19 AM | 0 comments

REAL Madrid imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Atletico Madrid katika mchezo wa kwanza wa Super Cup ya Hispania usiku wa jana Uwanja wa Santiago Bernabeu.
Msambuliaji Crisitiano Ronaldo alitolewa kipindi cha pili kumpisha mchezaji mpya, James Rodriguez, kabla ya Mcolombia huyo kuifungia bao la kuongoza Real dakika ya 81.
James Rodriguez aliingia kuchukua nafasi ya Ronaldo na kwenda kufunga

Atletico Madrid ilikomboa bao hilo zikiwa zimesalia dakika tatu kupitia kwa Raul Garcia na sasa Real Madrid itakabiliwa na mtihani mgumu katika mchezo wa marudiano Uwanja wa Vicente Calderon.
Kikosi cha Real Madrid kilikuwa: Casillas, Carvajal, Pepe, Ramos, Marcelo, Modric, Kroos, Alonso, Bale, Ronaldo/Rodriguez dk45 na Benzema.
Atletico Madrid: Moya, Juanfran, Miranda, Godin, Siqueira, Mario, Gabi, Koke, Saul/Griezmann dk56, Raul Garcia, Mandzukic.

Share story hii kupitia>>>>>> :
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Category:

0 comments