WATANZANIA HATUJACHELEWA KUFAHAMU NAMNA MAJUKUMU YA MABEKI WA PEMBENI YALIVYOBADILIKA......
Siku
za karibuni nimekuwa nikifuatilia mechi za ligi kuu ya Vodacom hapa
nchini, miongoni mwa maeneo ambayo baada ya kufuatilia kwa muda mrefu
sasa nimegundua yanahitaji sana maboresho ni sehemu ya mabeki wa
pembeni.
Kutokana na mabadiliko makubwa ya namna ya uchezaji siku hizi, imepelekea pia majukumu ya wachezaji kiwanjani kubadilika kutokana na mahitaji ya kisasa tofauti na ilivyokuwa hapo mwanzoni. Juzi nilikuwepo kwenye uwanja wa Chamazi kuwashuhudia wawakilishi wetu Azam FC kwenye kombe la shirikisho walipokuwa wanacheza na timu ya Feroviarrio kutoka kule Beira nchini Msumbiji.
Pamoja na Azam kupata ushindi wa bao 1-0 niligundua mabeki wa pembeni Malika Ndeule na Erasto Nyoni kama wangecheza kama ambavyo mahitaji ya mchezo wa kileo yanavyowataka wabeki wa pembeni kucheza basi Azam wangeweza walau kupata ushindi zaidi ya walioupata ama kwenye mechi ya marudiano wakirekebisha hayo mapungufu basi watakuwa na nafasi ya kusonga mbele kwenye mashindano hayo.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi1qD-bH7OZYINsKQXX3VpCIU3QtPViiWVklrQpbFnuXfBQD069dQ4zZSv4IWukEZxuLtr3Xb-T_iABWve15nExI99JvZU9vsE0zVlZu1iTrAfZXyAbgt-n3_wYuKMUJo1jnjnJZfUuRZ4/s1600/DSC_0020.JPG)
Katika kuelezea jukumu la beki wa aidha upande wa kushoto au kulia, kazi yao kubwa ni kulinda goli lao kwenye pembe za uwanja, wakiwazuia wachezaji wa timu pinzani kuingiza mipira ndani ya eneo lao penati na kuleta madhara.
Jukumu lao la pili, pia wanatakiwa kusaidia timu wakati wa kushambulia.
Kutokana na mabadiliko makubwa ya namna ya uchezaji siku hizi, imepelekea pia majukumu ya wachezaji kiwanjani kubadilika kutokana na mahitaji ya kisasa tofauti na ilivyokuwa hapo mwanzoni. Juzi nilikuwepo kwenye uwanja wa Chamazi kuwashuhudia wawakilishi wetu Azam FC kwenye kombe la shirikisho walipokuwa wanacheza na timu ya Feroviarrio kutoka kule Beira nchini Msumbiji.
Pamoja na Azam kupata ushindi wa bao 1-0 niligundua mabeki wa pembeni Malika Ndeule na Erasto Nyoni kama wangecheza kama ambavyo mahitaji ya mchezo wa kileo yanavyowataka wabeki wa pembeni kucheza basi Azam wangeweza walau kupata ushindi zaidi ya walioupata ama kwenye mechi ya marudiano wakirekebisha hayo mapungufu basi watakuwa na nafasi ya kusonga mbele kwenye mashindano hayo.
Katika kuelezea jukumu la beki wa aidha upande wa kushoto au kulia, kazi yao kubwa ni kulinda goli lao kwenye pembe za uwanja, wakiwazuia wachezaji wa timu pinzani kuingiza mipira ndani ya eneo lao penati na kuleta madhara.
Jukumu lao la pili, pia wanatakiwa kusaidia timu wakati wa kushambulia.
Mwanzoni,
mabeki wa pembeni walikuwa wagumu na kuaminika sana, jukumu kubwa na la
pekee lilikuwa kusimamia ulinzi zaidi, lakini siku hizi timu nyingi
zimekuwa na mabeki wa pembeni ambao wamekuwa wasaidizi wazuri wa
mashambulizi ya timu zao kutokea pembeni.
Kwa
kipindi cha miaka 10 iliyopita majukumu ya mabeki wa pembeni
yamebadilika. Hivi sasa, timu nyingi bado zinacheza na mabeki wazuri wa
pembeni ambao wanaweza kuzuia vizuri pamoja na kushambulia, mfumo wa
siku hizi mabeki wa kati wanajipanga kucheza pembeni kuhakikisha
wanakuwa na mstari mzuri wa ulinzi. Lakini hii staili haipo kwa timu
ambazo zina uwezo mdogo wa kumiliki mpira, ambazo muda mwingi wa mchezo
zinakuwa zinazuia mashambulizi, hivyo zinakuwa hazihitaji mabeki wao wa
pembeni kwenda mbele kushambulia - staili hii inaweza kuonekana sio
nzuri hasa kwa sababu inaacha mstari wa ulinzi hasa kati kati kuwa wazi
wakati timu inapopoteza mpira.
Jukumu
la beki wa pembeni wa kisasa kwa ujumla kwenye timu inayocheza soka la
kushambulia na kwa timu inayocheza soka kwa kumiliki zaidi mpira, ni
kujenga mashambulizi kuanzia nyuima.
Jukumu
la beki wa pembeni limebadilika hasa wakati timu zilipoamua kucheza kwa
kumiliki zaidi mpira, hasa katika ligi kama ya Hispania ambapo timu
zinajaza viungo kati kujaribu kuimiliki zaidi mechi.
Mabeki
wa pembeni ndio wanategemewa zaidi kuipeleka timu mbele kwa sababu mara
nyingi ndio wachezaji wanaokuwa na nafasi kubwa uwanjani kwa sababu
katikati mwa uwanja kunakuwa kumejaa wachezaji wengi. Kwa
timu kuweza kufaidika na mfumo huu, mabeki wa pembeni inabidi wawe fiti
vya kutosha ili waweze kushambulia kutokea pembeni na kuwahi kurudi
wakati timu yao inashambuliwa.
Matokeo
ya mfumo huu timu nyingi zimeacha kuweka umuhimu wa kutumia mawinga
asilia. Kwa timu ambazo hazichezi na mawinga asilia, mabeki wa pembeni
ndio hutumika kama mawinga na mabeki kwa wakati mmoja.
AC
Milan wamekuwa maarufu kwa miaka kadhaa sasa kwa kucheza bila mawinga
asilia na wakiwa na mabeki wanaoshambulia. Kasi na nguvu ndio vitu
muhimu kwa mabeki wa pembeni wa kisasa kwa sababu watakuwa wanakimbia
eneo kubwa ikiwa watakuwa wanaifanya vizuri kazi yao.
Kutokana
na sifa hizi anazotakiwa kuwa nazo beki wa pembeni wa kisasa, ndio
maana sio jambo la kushangaza kuona kuna wachezaji wachache wanaoweza
kucheza kwenye nafasi hizo ukifananisha na sehemu nyingine dimbani.
Mabeki
wengi wa pembeni wa kisasa waliwahi kuwa wachezaji wa kushambulia ambao
walirudishwa nyuma kucheza kama mabeki wa pembeni. Mfano mzuri ni
wachezaji kama Ashley Cole, Patrice Evra, Daniel Alves na Zambrotta.
Jukumu la beki wa pembeni limekuwa kubwa kiasi kwamba katika michezo
mikubwa na muhimu, timu nyingi zimekuwa zikijaribu kuzuia kipekee mbio
za mabeki wa pembeni, huku timu nyingine zikitoa uhuru wa kushambulia
kwa mabeki wao. Kwa mfano, barani ulaya Manchester United inapendelea
kucheza na mawinga wazuiaji kama vile Antonio Valencia na hata Park
alitumika hivyo hivyo, hii ilikuwa kuweza kurudi na kusaidia kuzuia
mashambulizi ya wachezaji wa pembeni wa timu pinzani.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEixC-5Yd3z2EEgoCa2XWVgQo2D3WyeLWmF4_O-bMBjNQ9ljl79o_lR-brGaexuxKzQcr9M57KwA2RFbqlshy6COpT-N231lsJeOcIk5CtGqW-pCTCY6OQdJuWc4ZsMLffh0wZFi2d6ew4U/s1600/Daniel+Alves+Getafe+CF+v+Barcelona+ALAcYAWvLQ5l.jpg)

Daniel
Alves ni mfano wa beki wa pembeni ambaye timu inajipanga kwa mtindo wa
kipekee ili kuweka mfumo unaomfaa yeye na uchezaji wake. Ni mzuri sana
katika kushambulia, na kasi na nguvu - akiongeza mashambulizi ya Barca
kutokea upande wa kulia, hivyo mara nyingi Barcelona kucheza wachezaji
watatu mbele (hasa upande wa kulia) ili kwenda sawa na aina ya uchezaji
wake. Hii haiwapi shida Barcelona kwa sababu muda mwingi wa mchezo
wanakuwa na mpira wao; hii inamfanya Alves kuwa na faida sana kwenye
mashambulizi ya timu.
Hii
staili ya uchezaji timu nyingi bado hazijaimudu na ni vigumu kuweza
kuitumia katika siku za hivi karibuni, lakini kutokana na kuongezeka kwa
umuhimu wa mabeki wa pembeni leo hii, jukumu hili la mabeki wa pembeni
litazidi kuendelea kuboreka na litakuwa jambo la kawaida kiasi kwamba
timu zitakuwa zikipanga mbinu za kuzuia mashambulizi ya mabeki wa
pembeni zaidi ili kuweza kudhibiti mchango wao katika timu zao kuliko
ilivyo hivi sasa.
Imechotwa: shafiidauda.com
Category: tanzania
0 comments